Wednesday, 18 June 2014

TUJIFUNZE MAANDIKO

biblia photo: gif biblia animatedbook.gif 1.MAVAZITUVAAYO YANA UTUKUFU KWA MUNGU WETU
        
A.MAVAZI YA KIDUNIA                                         
 MITHALI 7:10 
                                “Na tazama, mwanamke akamkuta ana mavazi ya kikahaba”. Kwa muda mrefu, katika kanisa la Mungu duniani, wakristo wengi wamegubikwa na utata mwingi kuhusiana na somo la mavazi. Maswali yafuatayo yamekuwa yakiulizwa bila kupata majibu sahihi:-
Je, mkristo anaweza kuvaa vazi lolote alipendalo?
Je, Mungu anaangalia moyo tu na haangalii mambo ya nje kama mavazi?
Katika somo hili la mavazi ya kikahaba lililojaa wingi wa mafunuo ya kipekee, unaweza kupata majibu ya maswali haya na mengi mengine; kwa kina, mapana, marefu, kwa ufasaha mkubwa. Katika somo hili utapata maarifa ambayo kila mtu anayeokolewa anapaswa ayapate katika uchanga wake wa kiroho ili aweze kuwa tofauti na watu wa dunia (mataifa). Ili aweze kuwa nuru au barua inayosomeka vizuri 1.MAVAZITUVAAYO YANA UTUKUFU KWA MUNGU WETU
        
A.MAVAZI YA KIDUNIA                                         
 MITHALI 7:10 
                                “Na tazama, mwanamke akamkuta ana mavazi ya kikahaba”. Kwa muda mrefu, katika kanisa la Mungu duniani, wakristo wengi wamegubikwa na utata mwingi kuhusiana na somo la mavazi. Maswali yafuatayo yamekuwa yakiulizwa bila kupata majibu sahihi:-
Je, mkristo anaweza kuvaa vazi lolote alipendalo?
Je, Mungu anaangalia moyo tu na haangalii mambo ya nje kama mavazi?
Katika somo hili la mavazi ya kikahaba lililojaa wingi wa mafunuo ya kipekee, unaweza kupata majibu ya maswali haya na mengi mengine; kwa kina, mapana, marefu, kwa ufasaha mkubwa. Katika somo hili utapata maarifa ambayo kila mtu anayeokolewa anapaswa ayapate katika uchanga wake wa kiroho ili aweze kuwa tofauti na watu wa dunia (mataifa). Ili aweze kuwa nuru au barua inayosomeka vizuri tofauti na jinsi alivyokuwa mwanzo kabla hajaokolewa (MATHAYO 5:16; 2WAKORINTHO 3:2-3).
Siku hizi za mwisho, tumekuwa na walimu wengi katika kanisa la Mungu ambao hufundisha kuwa Mkristo anaweza kuvaa vyovyote vile kwa hoja mbalimbali. Kabla hatujaziangalia hoja zao, hatuna budi kufahamu hili kwanza. Mungu ametahadharisha juu ya kuwepo kwa walimu wengi wa uongo. Kumbuka neno WENGI (2 PETRO 2:1-3; MATHAYO 24:11). Hukumu ya walimu wa uongo itakuwa kubwa sana ( YAKOBO 3:1). Hatuna budi kujua kuwa wote tutahukumiwa sawasawa na injili ya Paulo mtume (WARUMI 2;16). Paulo mtume anasema, injli inayohubiriwa kinyume na injili yake ni injli ya namna nyingine (WAGALATIA 1:6-9). Yeyote anayehubiri injili kinyume na injili ya Paulo mtume amelaaniwa na hawezi kuingia mbinguni (MATHAYO 25:41).Tukijua kuwa tumezungukwa na upepo wa elimu ya uongo (WAEFESO 4:14), tunapaswa kuchunguza maandiko kwa umakini. Watu wa Beroya, waliyachunguza maandiko kuona kama ndivyo yalivyo wakati Paulo na Sila walipokuwa wakiwafundisha (MATENDO 17:10-11). Maana hatuwezi kutenda neno lolote kinyume cha kweli, bali kwa ajili ya kweli (2WAKORINTHO 13:8). Kweli ni Neno la Mungu (YOHANA 17;17). Zifuatazo ni hoja za baadhi ya walimu wanaofundisha Neno la Mungu:-

HOJA YA KWANZA
Mungu haangalii mambo ya nje, anaangalia mambo ya ndani. Wanafundisha wakisema mavazi hayawezi kumzuia mtu kuingia mbanguni. Wanawatia moyo watu waendelee kuvaa mavazi wapendavyo bila kuangalia maandiko yanavyosema    
Tunapaswa kujua kuwa utakatifu ni mwili na roho siyo ndani tu kama wao wasemavyo (1 WAKORINTHO 7:34; 2 WAKORINTHO7:1;  1WATHESALONIKE 5:23). Bwana Yesu alifundisha juu ya utakatifu kwamba unaanzia ndani na kasha nje. Hapo ndipo tunakuwa tumeutimizav utakatifu mwili na roho (MATHAYO 23:25-26). Yesu alisema “tutawatambua kwa matunda yao” (MATHAYO 7:15-21).Mtihutambulika kwa matunda yake. Matunda hayakai ndani ya mti, huwa nje ya mti. Hivyo, mavazi yanaweza kumtambulisha mtu, yeye ni nani na  kazi yake ni ipi. Hata kwa kahaba ni hivyo (MITHALI 7:10).

 HOJA YA PILI
Tuko huru ndani ya Yesu. Palipo na roho wa Mungu ndipo penye uhuru (WAGALATIA 5:1; 2WAKORINTHO 3;17). Hatuna budi kujua, kabla hatujaokolewa tulikuwa watumwa (YOHANA 8:33-36). Anachozungumzia Yesu ni uhuru mbali na dhambi (WARUMI 6:16-18). Baada ya kuokolewa sisi tunakuwa watumwa wa haki. Kwa hiyo, uhuru unaozungumziwa siyo wa kuvaa chochote au wa kufanya chochote kinyume cha Neno la Mungu.
HOJA YA TATU
Hatuko chini ya sheria wakati huu wa neema. Hatuna budi kufahamu kuwa, dhambi ni uasi wa sheria. Bila kuiasi sheria wewe si mwenye dhambi(1 YOHANA 3:4). Walimu hao, hutumia maandiko haya (WAGALATIA 5:4-5; ; WARUMI 6:14; WAGALATIA 5:18). Tunapaswa kufahamu kuwa, tumeokolewa na kutoka katika sheria ya Musa (WAEBRANIA 10:28). Hii ndio huitwa kongwa la utumwa. Tumetolewa kuwa chini ya sheria ya Musa na kuwekwa chini ya sheria ya Kristo (WAGALATIA 6:2). Sharia ya Kristo ni ngumu kuliko sheria ya Musa (MATHAYO 5:27-44). Sheria ya Yesu ni sheria ya Kifalme (YAKOBO 2:8). Sheria ya kifalme siyo ya kuchezea. Mfalme akiagiza jambo hana mjadala.
HOJA YA NNE
       Tuvae vyovyote ili tuwapate na mataifa. Walimu hao wanaamua kushusha viwango na  kujaribu kurahisisha njia ya kwenda mbinguni(1 WAKORINTHO 3:11). Msingi umekwisha kuwekwa ambao ni Yesu Kristo. Yesu ni mchungaji mkuu, wachungaji wote wako chini ya mchungaji huyo. Wachungaji wanapaswa kujifunza kwa mchungaji mkuu Yesu Kristo (WAEBRANIA 13:20). Alionesha kielelezo kwa kutokushusha viwangop vya mafundisho ili kuwa na idadi kubwa ya washirika  (YOHANA 6:61, 66-68). Wengi miongoni mwa wanafunzi wake walirejea nyuma na wasiambatane naye ( Yesu ) tena. Kilichowafanya kukwazika ni mafundisho magumu kutendea kazi ( Neno gumu ). Yesu kristo ili kuonesha mfano kwa wachungaji wa sasa, yeye hakuchuja Neno lake ili waendelee kuwepo bali hata wale wachache (tenashara/mitume) aliwageukia na kuwauliza kama na wao wanataka kuondoka..Alikuwa tayari kubaki peke yake na kuanza kazi upya. Tunaweza kuwa na orodha ndefu ya majina ya washirika waliojiandikisha  kanisani lakini majina hayo yakawa hayapo katika kitabu cha majina ya Mungu (kitabu cha uzima). Hatuwezi kuwaingiza watu mbinguni kwa viwango vyetu wenyewe, ni kwa kuongozwa na Neno la Mungu tu.
Wakitoka ndipo tunapojua kuwa hawakuwa wa kwetun(1 YOHANA 2:19). Sharti kanisa liongezeke kwa watu wanaookolewa na si vinginevyo (MATENDO 2:47). Mtu aliyeokolewa, amri za Mungu siyo nzito kwake (1YOHANA 5:1-5). Tunapaswa kujua kuwa watakaoingia mbinguni hawatakuwa wengi ukilinganisha na watakaotupwa motoni (MATHAYO 7: 13-14). Mataifa watutambua kuwa tumeokoka kwa matendo yetu          (1 PETRO 2:12;  2WAKORINTHO 3:1-3; MATHAYO 26:69-73).

MAJUM
Ujira  au mshahara wa kahaba na hanithi hautakiwi kupokewa ndani ya nyumba ya Mungu (Torati 23:17-18). Kama biblia inataja juu ya kuwepo kwa mavazi ya kikahaba, hatutakiwi kupuuzia.. Mtu akiokoka anapaswa kubadilika kwa kuyafanya matendo yanayoambatana na kutubu kwake (MATENDO 26:20). Tunapaswa kuzaa matunda na yaonekane (MATHAYO 3:8). Tukikosa ushuhuda mzuri, tunawafungia wengine kuingia katika ufalme (MATHAYO 23:13). Watu wanaookoka wanatoka katika mazingira na hali tofauti hivyo tunatakiwa kuwafundisha ili waishi sawa na viwango vya Neno la Mungu. Pia desturi na tamaduni zetu zinaweza kuwa kinyume na Neno la Mungu kwa sababu waanzilishi wake wengine hawajaokoka. Neno linasema tusifuate nasaba zisizo na ukomo. Nasaba ina maanisha tamaduni. (1 TIMOTHEO 1:3-4). Mavazi ya kikahaba yanakuwa na lengo la kuwavuta hao tunaotaka kufanya nao uchafu.
        Ifuatayo ni misingi inayotupa kujua  mavazi ya kikahaba.
  • MSINGI WA KWANZA
           HATUTAKIWI KUBADILI MATUMIZI YA ASILI.
Mungu anasema katika Neno lake “wala msimpe Ibilisi nafasi” (WAEFESO 4:27). M,apepo yana uwezo wa kufanya uzinzi au uasherati na binadamu. Yanaweza kuja kwa namna mbalimbali (WALAWI 17:7). Waathirika wakubwa wa nguvu za giza (mapepo na majini ) ni wanawake na mgogoro mkubwa ni kwenye mavazi ya kikahaba. Mavazi ya kikahaba ni mlango mkubwa wa mashetani kuwashambulia watu. Kubadili matumizi ya asili ya viungo vya binadamu yawe yasiyo ya asili nyuma yake kuna mashetani. Tukifanya hivyo tutakuwa tunampa nafasi Ibilisi  (MWANZO 19:1-28; YUDA 1:6-8). Wakati wa Ruthu katika mji wa Sodoma na Gomora na miji jirani, walifanya uchafu wa kila namna wanaume na wanawake wakiwakiana tama lakini nyuma yake yalikuwepo mashetani (YUDA 1:6-8) “Wakaendelea kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili”. Kumbe kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili nyuma yake kuna mashetani. Kazi ya shetani ni kuharibu mpango wa Mungu wa uumbaji, mpango wa Mungu wa maumbile (YOHANA 10:10). Mtu akipagawa na mashetani ndipo anaanza kuharibu mpango wa Mungu kwa kufanya mambo yasiyo ya asili (MARKO 5:1-20; WARUMI 1:26-28). “Mungu akaona kila alichokifanya (kiumba) na tazama ni chema (kizuri) [MWANZO 1:31]. Shetani anatupandikizia mawazo mabaya tuone kuwa Mungu alikosea katika uumbaji wake. Anatufanya tuone nywele za wazungu ni nzuri sana kuliko zetu waafrika. Pia anatufanya tuone rangi ya ngozi yao ni nzuri kuliko yetu hii nyeusi n.k.  Kufanya kinyume na uumbaji wa Mungu wa  maumbile yetu ni kumsahihisha Mungu. Kiumbe kinamuona yeye aliyekiumba hana ufahamu. Kitendo hicho ni sawa na kutaka kumpindua Mungu kwenye kiti chake cha enzi. Ni dharau ya hali ya juu (ISAYA 29:16; WARUMI 9:19-21). Ujasiri wa kumdharau Mungu unatoka wapi? Bila shaka unatoka kwa shetani. Mungu anasema “Wao  wanaoniheshimu nitawaheshimu na wanaonidharau watahesabiwa kuwa si kitu (1 SAMWELI 2:30).
UHISHO

B.
  MAVAZI YA MTU ALIYEOKOKA
Yesu ametuagiza watu tuliookoka katika MATHAYO 5:16,akisema, “Vivyo hivyo nuru yenu iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni”. Ni muhimu kufahamu kwamba watu ambao hawajaokoka ingawa hawafahamu kwa undani mafundisho ya Biblia, lakini wanajua sana kipi ambacho hakifai mbele za Mungu; kwasababu kazi ya Torati au Biblia, imeandikwa mioyoni mwao na dhamiri yao kuwashuhudia (WARUMI 2:14-15). Ndiyo maana mataifa wanajua  kwamba wizi, rushwa, magendo, kutoa mamba, kulewa au kuvuta sigara, uasherati au uzinzi, masengenyo, uongo, n.k. vyote hivi ni dhambi, ingawa ukiwauliza maandiko hawajui. Hatuwezi kamwe kuangaza  mbele yao ikiwa tunavaa mavazi ambayo wanajua kwamba ni mavazi yasiyompasa mtu anayesema ameokoka. Ni kwasababu hii, leo tunajifunza kuhusu mavazi ya mtu aliyeokoka;  na tutaligawa somo letu katika vipengele vine:-
( 1 ). UTAKATIFU MWILI NA ROHO
( 2 ). JINSI MAVAZI YANAVYOMTAMBULISHA MTU
( 3 ). AGIZO LA MUNGU LA KUTOKUFUATISHA NAMNA YA DUNIA HII
( 4 ). MISINGI SITA YA KUFAHAMU MAVAZI YANAYOTUPASA KUVAA                                          WATU TULIOOKOKA

( 1 ).  UTAKATIFU MWILI NA ROHO
Watu wengine kwa kutokufahamu, wanafikiri kwamba utakatifu ni katika roho tu na kwamba eti Mungu anaangalia ndani tu, haangalii nje. Hii siyo sahihi kulingana na maandiko. Yesu anasema  “safisha kwanza ndani…………ili nje yake nayo ipate kuwa safi ( MATHAYO 23:26 ). Unaona, ni suala la ndani na nje.Utakatifu ni yote yanayohusiana na mwili unaoonekana nje, na roho inayoonekana ndani                               ( 1 WAKORINTHO 7:34; 2 WAKORINTHO 7:1 ). Yale ambayo mataifa watayaona kwetu ni yale ya mwili yaani ya nje na siyo ya roho wasiyoweza kuyaona kwa macho. Mtu aliyeokoka anatambulika kwa matunda yake na matunda ya mti huonekana nje ya mti siyo ndani ( MATHAYO 12:33 ).

( 2 ). JINSI MAVAZI YANAVYOMTAMBULISHA MTU.
Mavazi yana sehemu kubwa sana katika jamii, katika kumtambulisha kwamba yeye ni nani, ana tabia gain n.k.Kuna usemi wa kiingereza unaosema, “what you wear, tells what yourare”. yaani, “mavazi yako yanaeleza waziwazi  kwamba wewe ni nani”. Kutokana na mavazi ya mtu, tunaweza kumtambua mtu huyo kwamba ni askari polisi au wa usalama barabarani, askari wa magereza, J.K.T, au Jeshi la wananchi, Daktari au Nesi, mwanafunzi au makenika, motto mdogo au mtu mzima., mwendawazimu au mwenye akili timamu n.k. Tukimwona mtu mzima barabarani amevaa nepi, tutajua huyo ni mwendawazimu. Tukimwona mkulima analia huku amevaa suti, tutajua pia kuwa huyo ni mwenda wazimu n.k. Mavazi yanamfanya mtu  adhaniwe kwamba ni kahaba ( MWANZO 38:15 ) Mavazi ya Musa ambaye ni Mwebrania au Mwisraeli, yalimfanya aitwe Mmisri (KUTOKA 2:17-19). Watu tuliookoka, tunaweza kuitwa Wamisri au watu ambao hawajaokoka kutokana na mavazi yetu.

“ wala msifuatishe namna ya dunia hii………..( WARUMI 12:2 )”,ni agizo la Mungu kwetu tuliokoka. Kuwa rafiki wa dunia yaani kuwa kama watu wa dunia, ni kuwa adui wa Mungu (YAKOBO 4:4 ). Hatupaswi kabisa kuzifuata njia za mataifa katika kufanya jambo lolote ( KUMBUKUMBU LA TORATI 18:9; 2WAFALME 17:8-11; 21:2; ZABURI 106:35; YEREMIA 10:2; WAEFESO 4:17 ). Kuna namna ya dunia au mataifa katika mavazi, hatupaswi kuifuatisha. Shetani ni mungu wa dunia hii ( 2WAKORINTHO 4:4 ). Atafanya kila namna kutufanya sisi  tuliookoka tuwe kama watu wa dunia katika mavazi ili tuwe adui wa Mungu. Tukifanya hivi kanisa la Mungu litanyonywa nguvu yake na hatuwezi kuwatiisha Mataifa kwa neno au kwa tendo kutokana na ishara na maajabu ( WARUMI 15:18-19 ). Hatuwezi pia kuwa barua au waraka wa injili unaosomeka kwa mataifa, ( 2 WAKORINTHO  3:2-3 ), Tutawanyoshea kidole kimoja vitaturudia vidole vine.
( 4 ).  MISINGI SITA YA  KUYAFAHAMU MAVAZI YANAYOTUPASA KUVAA WATU TULIOKOKA.
1. Mavazi  ni ya kuficha uchi-Mapambo yoyote hayatakiwi.
Kusudi la Mungu kutupa mavazi ni kuficha uchi wetu (MWANZO 3:21 ). Mapambo yoyote au Vyombo vya uzuri ni machukizo mbele za Mungu ( KUTOKA 33:4-6; HOSEA 2:13; EZEKIELI 23:26-30,40,42; YEREMIA 4:30 ).. Hatupaswi kuyaridhia mafundisho ya Yezebeli mwanamke aliyejipamba kwa uwanja machoni na kupamba kichwa na hatimaye akafa kifo cha kuhuzunisha ( 2 WAFALME 9:30-37; UFUNUO 2:20 ). Heleni au  pete za masikio, dusumali yaani mapambo ya kichwa, vikuku na mafurungu yaani aina zozote za bangili, pete, azama ( pete za puani ), vioo ( miwani ya jua ), marashi, mishipi mikubwa ( fingerbelt ), rangi za macho, midomo au kucha, wanja za macho, mikufu au chain, shanga za aina yoyote, mapambo ya dhahabu yoyote iwe ni mikanda ya saa ya dhahabu au mishipi ya dhahabu, vyote siyo vya lazima na ni machukizo mbele za Mungu ( ISAYA 3:16-26; 1TIMOTHEO 2:9; 1PETRO 3:3-5). Mishipi ni vazi  ( YEREMIA 13:1-2 ), lakini inapokuwa mikubwa kiunoni tayari ni namna ya dunia. Kujipaka marashi au manukato ya kutufanya tunukie kila mahali ni namna ya dunia hii. Yesu alimiminiwa marhamu au manukato ikiwa ni utabiri wa kuzikwa kwake (MATHAYO 26:7-12). Desturi ya wayahudi katika kuzika ilikuwa kuuzongazonga mwili wa maiti pamoja na manukato na madawa ili usinuke maana walikuwa wanakuja kuuangalia. Pia makaburi yao yalikuwa yanachongwa mwambani (YOHANA 19:38-40; MARKO 16:1; 2NYAKATI 16;13-14; MWANZO 49:33-50; 50:26 ). Dhahabu ni nzuri lakini siyo kwa ajili ya mapambo bali ni kwa ajili ya kutengenezea vyombo kama vya hospitali, katika eropleni n.k, ambavyo vinahitaji madini laini ( soft metal ). Wakati Mariamu na Yusufu alipopewa dhahabu kama zawadi kwa mtoto Yesu  ( MATHAYO 2:11 ), haikuwa kwa ajili ya mapambo ya Mariamu, bali kwa ajili ya gharama ya kuondoka Bethlehemu mpaka Misri na kuweza kuishi huko ugenini mpaka Herode alipofariki. Dhahabu ilitumika kama fedha yenye dhamani na iliwasaidia maskini Mariamu na Yusufu. Hekalu la Sulemani lilijengwa kwa dhahabu likaja kuvunjwa ili Mungu atufundishe kwamba hatasita kumwadhibu yeyote.Musa hakuingia Kanaani, hata kama mtu ni tajiri mkubwa ataanguka hukumuni pasipo wokovu ( ZABURI  49:16-20 )
2.  Mavazi ya kukosesha ni machukizo kwa Bwana ( MATHAYO 18:6-7 )
Ni wajibu wa wanawake kuwalinda wanaume kutokana na mavazi yao (YEREMIA 31:22 ). Mavazi yoyote ya kuonyesha ndani , mavazi mafupi yasiyoweza kufunika magoti mwanamke anapokaa, mavazi yanayoacha makwapa wazi yaani yasiyo na mikono, au yanayoacha kifua, tumbo au mgongo wazi, mavazi ya kubana, mavazi yenye matundu au yanayochanwa mbele au nyuma ili kuonyesha underskirt, kujifunga kanga bila kuvaa gauni na kuacha kifua na mgongo wazi, yote haya ni mavazi yanayokosesha wanaume siyo ya Kikristo. Wanaume kuvaa shati bila kufunga vishikizo na kuonyesha kifua hadharani au kufunga taulo na kuacha kifua wazi na kuonekana hadharani, kuvaa bukta hadharani, yote haya ni machukizo.
( 2 ).  Mavazi ya kututambulisha sisi sawa na Mataifa ni machukizo ( WARUMI 12:2 ). Mavazi yoyote ambayo yatatufanya tuonekane kama wahuni au mataifa siyo sahihi katika Ukristo. Jeans, Kadeti, mitindo yoyote ya mashono ya kihuni, viatu virefu vinavyotufanya tushindwe kukimbia na kuwa na mwendowa madaha ( ISAYA 3:16-17 ), kuning’iniza funguo na mafilimbi kwenye mkanda kama mapambo, mashati mapana au kofia za macheki bob n.k, yote haya ni machukizo. Ndevu za kutufanya tuitwe “Mzee Ndevu” au “Mzee Masharubu” tunapaswa kuziondoa.

( 4 ).  Mwanamke hana budi kuvaa mavazi ya kike na mwanamume mavazi ya kiume ( KUBUKUMBU LA TORATI 22:5 ).
Mwanamke hapaswi kuvaa suruali, bukta au kaputura. Brauzi zinazokuwa kama mashati ya kiume au fulana za kiume, mwanaume kuvaa kanga, wanaume kuvaa mikufu n.k., yote haya siyo sehemu ya Ukristo.
( 5 ).  Vaa kwa utukufu wa Mungu ( 1 WAKORINTHO 10;31 )
Hatuvai kwa  kushindana. Kuazimana nguo kwa lengo la mtu  kuonekana  ana nguo, siyo Ukristo. Kupamba kichwa ( 2 WAFALME 9:30 ), kwa kukali nywele, ku-relax kuweka rasta, kuchoma nywele n.k., siyo sehemu ya Ukristo. Mwanamke awe na nywele ndefu kama fahari yake kwa kuzitunza  kikawaida, mwanaume asiwe na nywele ndefu kama za kike ( 1 WAKORINTHO 11:14-15 ). Kwa  ajili ya malaika, mwanamke anaposali au kuomba au kuhubiri afunike kichwa kwakitambaa kisiwe chenye shanga  kama vitamba Arabuni. Hii pia ni kuonyesha dalili ya kumilikiwa na mwanamume ( 1 WAKORINTHO 11:5,8-13 ). Mwanamume wakati wa kusali au kuhubiri hapaswi kuvaa kofia ( 1WAKORINTHO 11:4,7 ).

( 6 ).  Maandishi katika mavazi yanapaswa kuwa yale tu ya kumtukuza Mungu (KUMBUKUMBU LA TORATI 11:18-21).
Kanga au T-shirt au nguo zozote tunazovaa ni lazima tuangalie maandishi yake. Maandishi ya kihuni kama “mtaa wa pili mtanikoma” “Mimi shangingi” “Sijui kosa langu” n.k., hatuna budi kuyafuta au kuyakata na kuyatoa katika kanga zetu na pia kanga zza jinsi hiyo hatupaswi kuziuza katika maduka yetu pamoja na mapambo yote. Vilevile mifuko ya plastiki iliyoandikwa “ MICHAEL JACKSON n.k.,haifai, kwa muhtasari, tuwe macho kuzijua hila za Ibilisi katika mavazi yetu. Anakuja kijanja sana. Saa zinazotoa sauti za muziki usio wa Kikristo ni namna ya dunia hii.

SOMO: 2.   VIZUIZI VYA NGUVU ITOKANAYO NA KUFUNGA

Somo letu la leo, ni somo la mwisho katika mfululizo wa masomo yahusuyo kufunga.  Ingawa kichwa cha somo letu ni “VIZUIZI VYA NGUVU ITOKANAYO NA KUFUNGA“, hiki kitakuwa ni kimoja kati ya vipengele vitatu tutakavyojifunza katika somo letu la leo:-
(1)      AINA MBILI ZA KUFUNGA;
(2)      KIPINDI CHA KUFUNGA;
(3)      VIZUIZI VYA NGUVU ITOKANAYO NA KUFUNGA.
(1)      AINA MBILI ZA KUFUNGA
Ziko aina mbili za kufunga ambazo kila mtu aliyeokoka anapaswa kuzishiriki:-

  1. KUFUNGA KUTOKANA NA MBIU YA KUFUNGA – (2 NYAKATI 20:3-4; YONA 3:7-8; EZRA 8:21). 
Huku ni kufunga kunakotokana na mbiu ya kufunga inayoletwa kwetu tufunge kwa siku kadha kwa ajili ya jambo fulani na kisha kukutana mahali fulani kwa ajili ya kilele cha maombi, hiyo ni mbiu ya kufunga.  Mbiu ya kufunga inaweza kutangazwa na Kiongozi wa Zoni, Kiongozi wa Kanisa la Nyumbani, Kiongozi wa Kikosi Maalum cha Maombi (Powerhouse), Kiongozi wa Kwaya n.k; na kiongozi huyo ataeleza makusudi ya kufunga huko.  Mbiu ya kufunga, huleta baraka kubwa kwa jinsi inavyojumuisha watu wengi kwa pamoja, wanaopatana kwa nia moja, katika kipindi kimoja, kuombea mambo fulani maalum.
  1. 2.     KUFUNGA KWA UAMUZI WA BINAFSI (NEHEMIA 1:4)
Katika maisha ya mtu aliyeokoka, mtu hujipangia binafsi vipindi vya kufunga na kuomba ili achote baraka zitokanazo na kufunga.  Kama kila mmoja anavyopasa kujipangia binafsi muda wake wa maombi bila kungojea maombi ya pamoja tu kanisani, vivyo hivyo, inampasa kila mmoja wetu kujipangia binafsi vipindi vya kufunga na kuomba, tukiomba kwa ajili ya wenye dhambi wamjue Mungu, kudhihirika kwa miujiza Siku ya Matendo ya Ajabu, tukiomba kwa ajili ya Mchungaji na viongozi wa Kanisa na kazi ya Mungu kwa ujumla katika Kanisa, n.k.
(2)      KIPINDI CHA KUFUNGA
Je tufunge kwa muda gani?  Biblia haiweki sheria juu ya siku ngapi za kufunga.  Hata hivyo, tukiangalia vipindi vilivyotajwa vya mfungo katika Biblia, tutaweza kujifunza mambo kadha.  Mifungo mingi katika Biblia, haitaji siku zilizotumika katika kufunga, lakini hapa tutaangalia ile iliyotajwa siku za mfungo na sababu za kufunga.
NA. ANAYEHUSIKA KUFUNGA KIPINDI CHA MFUNGO SABABU ZA KUFUNGA ANDIKO
1 DAUDI Asubuhi hadi Jioni. Kumuombolezea aliyekufa. 2 SAMWELI 3:35
2 ISRAELI Asubuhi hadi Jioni. Wakati wa Vita inaendelea kumwuliza Bwana juu ya kushindwa kwao.   WAAMUZI 20:24-27
3 DAUDI Asubuhi hadi Jioni. Kumlilia aliyekufa 2 SAMWELI 1:12
4 YUDA Siku moja nzima mchana na Usiku. Kuutafuta uso wa Mungu. NEHEMIA 9:1-4
5 YUDA Siku nzima. Kuutafuta uso wa Mungu. YEREMIA 36:6
6 FARISAYO Siku nzima mara mbili kwa juma kila wakati.
LUKA 18:9-12
7 ISRAELI Siku nzima. Kumlilia Bwana waokolewe na mkono wa Wafilisti. 1 SAMWELI 7:6-14
8 ESTA/MORDEKAI Siku tatu nzima. Kuutafuta uso wa Mungu ili kutoka katika matatizo. ESTA 4:13-16
9 WATU WENGI Siku tatu (3). Kumsikiliza Yesu akiwafundisha. MATHAYO 15:32
10 PAULO Siku tatu nzima (3). Wakovu na wito wa Paulo. MATENDO 9:9
11 DAUDI Siku saba (7). Kumwomba Mungu kwa ajili ya mtoto. 2 SAM. 12:16-18
12 ISRAELI Siku saba (7). Kuomboleza kifo cha Sauli na wanawe. 1 SAM. 31:13
13 PAULO NA WATU 276 Siku 14 nzima. Safari iliyojaa misukosuko. MATENDO 27:33,37
14 DANIELI Siku 21 nzima. Kumwomba Mungu baada ya kufunuliwa Neno. DANIELI 10:1-3
15 MUSA Siku 40 nzima. Kuketi mbele za Bwana mlimani na pia kuwaombea Waisraeli. KUMBUKUMBU LA TORATI 9:9, 18, 25-29; 10:10
16 YOSHUA Siku 40 nzima. Mlimani mbele ya Mungu. KUTOKA 24:12-15
17 ELIYA Siku 40 nzima. Safari ndefu baada ya chakula maalum. 1 WAFALME 19:5-8
18 YESU Siku 40 nzima. Kujaribiwa nykani kutokana na kuongozwa na Roho. MATHAYO 4:1-2

Kutokana na jedwali hili tunajifunza yafuatayo:-
1.         Kipindi cha kufunga katika kumtafuta Bwana kwa maombi, kinabidi kiwe  siyo chini ya siku moja (saa 24).  Kipindi kifupi chini ya hapo hutumika wakati wa vita inayoendelea ili kuhifadhi nguvu za vita kwa mfano kufunga wakati wa kulihubiri Neno la Mungu au kuhudumu.
2.         Kipindi cha kawaida cha mfungo hufikia siku tatu nzima.  Ni katika uzito usio wa kawaida tunazidisha hapo kwa maongozi ya Roho hata hivyo siku hazizidi saba.
3.         Kufunga zaidi ya siku saba lazima kuambatane na kufunuliwa neno.  Mtu hawezi kufunga siku 40 bila kula na kunywa mpaka kuwe na maongozi DHAHIRI ya Mungu kwake na uwepo wa Mungu na msaada wake maalum (1 WAFALME 19:8).
Mtendakazi mzuri wa Kristo atajipangia ratiba yake na kuwa na moja ya kumi ya siku za mwezi katika kufunga (siku tatu).  Inaweza ikawa siku moja katika wiki mara tatu na siyo mfululizo.
(3)      VIZUIZI VYA NGUVU ITOKANAYO NA KUFUNGA
            1.         NIA YA KUFUNGA (WARUMI 12:2)
Nia ya kufunga ikiwa siyo sawa na neno la Mungu, huzuia kupatikana kwa nguvu itokanayo na kufunga.
2.         KUFUNGA KATIKA DHAMBI (YEREMIA 14:10-12; ISAYA 58:3-5).
3.         KUFUNGA BILA KUOMBA – Kufunga lazima kuambatane na kumtafuta BWANA kwa maombi (2 NYAKATI 20:3-4; EZRA 8:21).
4.         KUFUNGA HAKUPASWI KUCHUKUA NAFASI YA IMANI – Hatupaswi kuwaza KILA jambo haliwezekani mpaka tufunge kwanza.  Pasipo imani ni bure (WAEBRANIA 11:6).  Kufunga kunachochea tu Imani.
…………………………………………………………………………………………………………………………………..
Ni sifa ipi ya kutuwezesha kuingia mbinguni?  Ni utakatifu (WAEBRANIA 12:14).  Ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge (UFUNUO WA YOHANA 21:27).  Kinyonge ni kipi?  Ni yule anayetenda dhambi.  Huyu ni mtu asiyefaa, ni mnyonge!  Je, wewe ni mtakatifu?  Jibu ni la!  Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini; hivyo wewe pia ni mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13;  YOHANA 14:6).  Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii?  Najua uko tayari.  Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni;  Mungu Baba asante kwa ujumbe huu.  Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi.  Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha.  Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo.  Bwana Yesu niwezeshe.  Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu.  Amen.  Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni.  Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.  MUNGU AKUBARIKI !!!

SOMO:  JINSI YA KULIELEWA NENO LA MUNGU
T
unaendelea tena leo, kujifunza Kitabu cha YOHANA katika Biblia zetu.  Leo tunatafakari YOHANA 7:17-52.  Ingawa kichwa cha somo letu la leo ni, “JINSI YA KULIELEWA NENO LA MUNGU“, kuna mengi zaidi ya kujifunza katika mistari hii.  Tutayagawa mafundisho yote tunayoyapata katika mistari hii, katika vipengele kumi:-

(1)      JINSI YA KULIELEWA NENO LA MUNGU 
(2)      JINSI YA KUMTAMBUA NABII WA KWELI 
(3)      KUSHINDWA KWA WANADAMU WOTE KUISHIKA TORATI 
(4)      SABABU KUU YA KUMWITA MTUMISHI WA MUNGU KWAMBA ANA PEPO 
(5)      WAJIBU NA JINSI YA KUHUKUMU 
(6)      SABABU KUU YA WATU WENGI KUSHINDWA KUMPENDA MUNGU 
(7)      SAA YA KUKAMATWA
(8)      NAMI NILIPO NINYI HAMWEZI KUJA
(9)      MITO YA MAJI YALIYO HAI 
(10)    KOSA LA KUMHUKUMU MTU KABLA YA KUMSIKIA 

(1)      JINSI YA KULIELEWA NENO la nyingi sana na kusambazwa na kusomwa kwa wingi, kuliko Kitabu chochote kile kingine ulimwenguni, katika wakati wote na miaka yote.  Kwa mfano, kulingana na vitabu vyenye takwimu, “ENCYCLOPAEDIA BRITANNICA“ na “ENCYCLOPAEDIA AMERICAN“, mwaka 1932 peke yake Biblia zilizoschapishwa na kusambazwa kwa lugha mbalimbali duniani, zilikuwa 1,330,213,815.  Miaka 50 iliyopita kulingana na mtafiti anayeitwa HY PICKERING, ili kukidhi mahitaji ya Biblia, Chama cha Biblia cha BRITISH AND FOREIGN BIBLE SOCIETY, kililazimika kuchapa nakala moja ya Biblia kila baada ya SEKUNDE TATU mchana na usiku au karibu nakala 32,876 kila siku katika mwaka mzima.  Biblia hizi zilisambazwa katika ulimwengu mzima kwa kutumia makasha 4,583 yenye uzito wa karibu TANI 500!  Hata hivyo, jambo la kushangaza ni kwamba mamilioni ya watu wanaosoma Biblia hawaielewi!  Tunajuaje kwamba hawaielewi?  Maisha ya watu hawa hayabadiliki na kufuata maelekezo ya Neno la Mungu.  Tatizo ni nini?  Jibu tunalipata katika MST. 17 “MTU AKIPENDA KUYATENDA MAPENZI YAKE (MUNGU), ATAJUA HABARI YA YALE MAFUNZO“.  Kama mtu hayuko tayari kulitenda kila jambo atakalofundishwa na Mungu katika Neno lake, Roho Mtakatifu humwacha mtu huyo, hawezi kumfunulia chochote katika Neno la Mungu.  Matokeo yake hawezi kuelewa lolote!  Bila roho Mtakatifu hatuwezi kufunuliwa na kulielewa Neno la Mungu (1 WAKORINTHO 2:10, 13; YOHANA 16:13).  Wengi wetu hatulielewi Neno kwa sababu hatuko tayari kulitendas.  Hatua yoyote ya kushindana na kupingana na Neno la Mungu, humfanya Roho Mtakatifu kutuacha mara moja.  Kabla ya kulisoma neno au kujifunza Neno la Mungu kwa njia yoyote, ili tulielewe Neno la Mungu, hatuna budi kuwa na msimamo wa kutaka kulitenda Neno lake sawasawa na (YEREMIA 42:1-6).

(2)      JINSI YA KUMTAMBUA NABII WA KWELI 
Yeye anenaye kwa nafsi yake tu, huyo siyo nabii wa kweli.  Kunena kwa nafsi yake mtu, ni kuhubiri au kufundisha kinyume na Neno la Mungu.  Mtu wa jinsi hii, hatafuti Utukufu wa Mungu, bali wake mwenyewe.  Nabii wa kweli humhubiri Kristo, au kwa jinsi nyingine, hulihubiri Neno! (WAFILIPI 1:18;  2 TIMOTHEO 4:2).

Wanadamu wote mble za macho ya Mungu, hakuna hata mmoja aliyeweza kuishika torati, maana mtu akiishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, anahesabiwa kukosa juu ya yote (YAKOBO 2:10).  Hivyo, mbele za Mungu, hakuna mwanadamu atendaye mema, la, hata MMOJA! (WARUMI 3:10, 12; 1 YOHANA 1:8).  Wanadamu wote tulistahili kuangikwa msalabani kama adhabu ya laana ya kutokuishika torati (WAGALATIA 3:10; KUMBUKUMBU 21:22-23).  Aliyempendeza Mungu sikuzote, na kufanya yaliyompendeza, ni Yesu Kristo pekee (MATHAYO 3:17; YOHANA 8:29).  Ni kwa sababu hii, tunahesabiwa haki BURE kwa neema yake, kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu kwa imani katika damu yake iliyomwagika msalabani, alipokufa kwa niaba yetu, ili awe upatanisho (WARUMI 3:24-26; 1 TIMOTHEO 2:5-6).

Mtumishi yeyote wa Mungu anayeyafichua maovu yaliyo……………………………. katika jamii ya watu wanaojiita Wakristo, na kuyanena waziwazi kwamba hayampendezi Mungu, na kuisema kweli, huyu sharti watu hao watamwita ana pepo.  Dhambi zinapokubalika katika Kanisa lote la Mungu na watu wanaojiita Wakristo, wanapokuwa hawana tofauti na wapagani au mataifa, anapoinuliwa Mtumishi wa Mungu na kuleta mageuzi, sharti mtu huyo ataitwa ana pepo.  Yesu hapa alifichua maovu yao na kuisema kweli kwamba wanataka kumuua, wao wakakana, wakaipinga kweli hiyo wakati ilikuwa kweli; kinyume chake wakamwita ANA PEPO, ili kujikosa na kuhalalisha maovu yao!  (MST. 19-20, 23).  Hivyo ndivyo inavyokuwa wakati awote.  Haya yalimpata Martin Luther, John Wesley, Charles Finney na wote walioleta mageuzi ya jinsi hii nyakati zao.

(5)      WAJIBU NA JINSI YA KUHUKUMU 
“Ifanyeni hukumu iliyo haki“, ni mafundisho ya Yesu Kristo kwetu.  Hatupaswi kukaa kimya kwa visingizio vya Neno, “Msihukumu“, na kuacha kuyakosoa mafundisho potofu ya Mashahidi wa Yehova; Mormonism au Christ Church for Latter Day Saints, wanaoshika mafundisho ya Joseph Smith; au wanaojiita Wakristo na kusema wao siyo dhehebu, wanaofuata mafundisho ya William Branham; au mafundisho yanayofundisha watu kushika sabato leo, au mafundisho mengine yoyote yaliyo potofu.  Kukaa kwetu kimya na kuogopa “kuyasema madhehebu mengine“, siyo kufuata nyayo za Mchungaji Mkuu wa Kondoo, Yesu Kristo na kufanya hivyo, ni kuwaachia kondoo wetu wararuliwe na mbwa mwitu.  Huo ni uchungaji wa mshahara.  Yesu aliifanya hukumu iliyo haki, pale alipokuwa kinyume na kuishika Sabato, na tena pale aliposema “Jilindeni na *chachu* au mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo“. (MATHAYO 16:11-12; YOHANA 10:12; MATENDO 20:28-30).  Tunapaswa kufuata kielelezo cha Yesu.  Kanisa la Kwanza walizingatia kufanya hivyo (WARUMI 16:17; 2 YOHANA 1:9-11).  Watu wenye mafundisho potofu, hatupaswi kuwa na ushirika nao, tuwahesabu tu kama mataifa na kuwahubiria kweli na kutokukubali kusikia chochote kutoka kwao.

(1)         SABABU KUU YA WATU WENGI KUSHINDWA KUMPENDEZA MUNGU
           
Tangu zamani za kale, sababu kuu ya watu wengi kushindwa kumpendeza Mungu, ni watu hao kuacha kumwamini Yesu na kuokolewa, kwa kungoja kwanza WAKUU WAMWAMINI (MST. 26).  Wengine wanangoja kwanza baba na mama, mume au kiongozi wao wa dini aokoke, ndiyo eti nao waokoke, na wanafuata mafundisho yao tu kimkumbo.  Huu ni mtego mkubwa wa Ibilisi.  Ukitengwa ugali mezani kila mtu huchukua tonge lake mwenyewe!  Ndivyo ilivyo, damu imemwagika msalabani, wokovu tayari.  Kila mmoja anapaswa kuuchukua kwa imani.  Ni muhimu kukumbuka pia kwamba, kila mtu atalichukua furshi lake mwenyewe na kutoa habari zake MWENYEWE (WARUMI14:12; WAGALATIA 6:5).  Hakuna haja ya kungoja wakuu waokoke ndiyo nasi tuokoke.  Kufa hakufuati nani wa kwanza kuzaliwa!.

(7)      SAA YA KUKAMATWA 
Maadui zetu watatutafuta sana ili watushike na kutudhuru, hata hivyo, hatupaswi kuhofu.  Hatuwezi kufa mpaka saa yetu itakapowadia.  Juhudi zao zitagonga mwamba, wakati wote Bwana wetu atatupa mlango wa kutokea maana amesema atakuwa pamoja nasi hat ukamilifu wa dahari yaani mwisho wa mambo yote (MATHAYO 28:19-20; AYUBU 5:20, 26-27).

(8)      NAMI NILIPO NINYI HAMWEZI KUJA 
Hatuwezi kumwona Yesu pasipo Utakatifu na kutafuta kwa bidii kuwa na amani na watu wote (WAEBRANIA 12:14).  Ni wale tu wenye mioyo safi watakaomwona Mungu (MATHAYO 5:8).  Ikiwa tumejaa masengenyo, chuki, fitina, hasira, mawazo machafu, n.k. tutamtafuta Yesu tusimwone.
(9)      MITO YA MAJI YALIYO HAI 
Mtu akimpokea Roho Mtakatifu, ishara ya kwanza itakayoonekana kwake, ni kunena kwa lugha mpya kadri roho atakavyomjalia kutamka (MATENDO 2:4; 10:44-46; 19:6).  Maji yanapokuwa yanapita katika mto, hutoa aina fulani ya sauti isiyoweza kuelezeka.  Ndivyo alivyo mtu anenaye kwa lugha baada ya kumpokea Roho, mito ya maji hutoka ndani yake!

(1)            KOSA LA KUMHUKUMU MTU KABLA YA KUMSIKIA KWANZA NA KUJUA
             ATENDAVYO 
Watu wengi hufanya kosa la kumhukumu Mtumishi wa Mungu kabla ya kumsikia kwanza anenavyo au anavyofundisha na kujua atendavyo.  Haitupasi kufanya hivi.  Watumishi waliotumwa na makuhani kumkamata Yesu, walikubali kwanza kumsikia na wakagundua kweli waliyokuwa wamefichwa na Shetani.  Kuna faida kubwa kuiga mfano wao.

SOMO:   TABIA NA KAZI ZA ROHO MTAKATIFU
S
iku ya leo ya Kuichambua Biblia, tunaendelea kujifunza Kitabu cha YOHANA katika Biblia zetu.  Leo, tutatafakari kwa makini YOHANA 16:5-22.  Katika mistari hii, pamoja na mambo mengine, tunajifunza, “TABIA NA KAZI ZA ROHO MTAKATIFU“.  Tutayagawa mafundisho yote tunayoyapata katika mistari hii katika vipengele vinne:-
(1)      YESU MWALIMU WA MFANO 
(2)      TABIA NA KAZI ZA ROHO MTAKATIFU 
(3)      HEKIMA YA KUWALEA WATOTO WACHANGA KIROHO 
(4)      HUZUNI KUGEUKA KUWA FURAHA

(1)         YESU MWALIMU WA MFANO 
Yesu Kristo, Mwalimu wetu, katika mstari huu, anawauliza wanafunzi wake, “Wala hakuna mmoja wenu aniulizaye, Unakwenda wapi?“.  Siyo kwamba wanafunzi wake walikuwa hawajauliza kabisa swali hili.  Petro aliuliza swali hili katika YOHANA 13:36, na Tomaso aliuliza swali lililokuwa na maana hiyo katika YOHANA 14:5.  Hata hivyo, baada ya wanafunzi hawa kuuliza swali hili mara mbili, hawakumwuliza tena.  Yesu alitaka wazidi kumwuliza, maana aliwaona bado hawajaelewa.  Hapa, Yesu anatoa mfano kwa Walimu wote wa biblia.  Furaha ya Mwalimu yeyote wa Biblia anayefuata mfano wa Yesu, ni kuona wanafunzi wake wanaelewa, na kuyatendea kazi yale wanayofundishwa.  Mwalimu wa Biblia, hataridhika kuona anafundisha tu wakati wanafunzi wake hawamwelewi.  Furaha yake itakuwa kuona wanafunzi wake wanauliza maswali tena na tena ili wapewe ufafanuzi kwa njia iliyo rahisi zaidi mapaka waelewe.  Mwalimu wa Biblia anayefuata mfano wa Yesu, hatachoshwa na maswali au kuyachukia, ikiwa wanafunzi hao watakuwa wanauliza maswali hayo kwa lengo la kutafuta kuelewa.  Sisi nasi kama wanafunzi wa Yesu, tunakumbushwa kuwa na bidii kuuliza maswali tena na tena, mpaka tuelewe, na kuishindania imani.  Wanafunzi wengi wa yesu, huona aibu kuuliza maswali na kuogopa kuonekana kuwa hawajui.  Kufanya hivyo kunatuweka katika hatari ya kuiacha imani kutokana na kutokuelewa, na kupata hasara ya milele.  Petro alikuwa mwulizaji mkubwa wa maswali.  Kutokana na maswali yake, tunapata mafundisho mengi ambayo tusingeyapata.  Kwa mfano, Petro bila aibu, anamwuliza Yesu katika MATHAYO 18:21  “Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nimsamehe? Hata mara saba?“  Kutokana na swali hili, wote tunapata mafundisho kuhusu kusamehe.

(2)         TABIA NA KAZI ZA ROHO MTAKATIFU 
Katika mistari hii, tunajifunza kuhusu tabia na kazi za Roho Mtakatifu.  Ingawa Roho Mtakatifu ana tabia na kazi nyingi zaidi kuliko zile zilizoorodheshwa hapa, hata hivyo, katika mistari hii, tunajifunza tabia na kazi zake za msingi.  Zifuatazo ni kazi za Roho Mtakatifu zinazotajwa katika mistari hii:-

  1. KUUHAKIKISHIA ULIMWENGU KWA HABARI YA DHAMBI: – Watu wote ambao hawamwamini Yesu, wanafanya dhambi (MST. 9).  Watu wengi ingawa hawamwamini Yesu, hujihesabia haki kutokana na amtendo yao kama Farisayo yule katika LUKA 18:9-14.  Watu wengi hujihesabia haki na kujiona kwamba hawana dhambi, kwa kuwa wanashika taratibu zote za dini zao, kama walivyofundishwa (MATENDO 26:4-5; WAGALATIA 1:14).  Kutokana na msingi huu, Sauli alijihesabia haki na kuona kwamba yeyote ambaye alikuwa hafuati taratibu zote za dini yake, ndiye mwenye dhambi na alifaa hata kuuawa.  Aliposikia sauti ya Yesu ikisema, Sauli! Sauli! Mbona waniudhi?  Alishangaa, maana aliona anatenda haki yote.  Tukitoka na kwenda kuwahubiria watu wa jinsi hii ya Farisayo na Sauli, na kutaka waokolewe, bila msaada wa Roho Mtakatifu, hatuwezi kufanikiwa, kwa sababu wao watajiona kuwa hawana dhambi na kutuona sisi ndiyo tuliopotea kwa sababu hatuko katika dini zao!  Mtu ambaye havuti sigara, hanywi pombe, haibi, hafanyi ushirikina, haui au hatukani matusi, mtu wa namna hii ni vigumu kumshawishi kwamba ana dhambi, na kumtaka atubu na kuokolewa, kwa kumfundisha tu kwamba, sisi sote tumefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu tangu kuzaliwa (ZABURI 51:5; WARUMI 3:10-12, 23; 1 YOHANA 1:8-10).  Sasa basi, ni kazi ya Roho Mtakatifu kumfanya kila mtu wa namna hii, anayejihesabia haki, kushtakiwa na dhamiri yake na kujiona hafai na ni mwenye dhambi (YOHANA 8:3-9).  Ndiyo maana, tukitoka kuwahubiri watu na kutegemea ujuzi wetu tu wa maandiko bila msaada wa Roho Mtakatifu, hatuwezi kupata matokeo makubwa.  Hatuna budi wakati wote kuitambua kazi hii ya roho Mtakatifu, na kumkaribisha aambatane pamoja nasi kila tunaposimama kuhubiri au kufundisha ili ashuhudie pamoja nasi (YOHANA 15:26-27).  Tukifanya hivi, huduma zetu zitakuwa na mafanikio makubwa.  Hatuna budi kupokea uwezo utokao juu, Nguvu ya Roho Mtakatifu ili tuwe mashahidi wa Yesu wenye uwezo wa kuwaleta wenye dhambi wengi kwa Yesu (LUKA 24:48-49; MATENDO 1:4,8).

  1. KUUHAKIKISHIA ULIMWENGU KWA HABARI YA HAKI: – Ni kazi ya Roho Mtakatifu kumhakikishia kila tunayemhubiri kwamba Yesu Kristo pekee ndiye mwenye haki na tunahesabiwa haki kwa kumwamini Yeye tu (1 YOHANA 2:1).  Roho Mtakatifu akitenda kazi hii humfanya mtu akiri kwamba Yesu ndiye mwenye haki, kama ilivyokuwa kwa akida katika LUKA 23:47.  Vivyo hivyo, Roho Mtakatifu huwahakikishia watu :  1.MAVAZITUVAAYO YANA UTUKUFU KWA MUNGU WETU         

  2. MSINGI WA KWANZA

  1. KUUHAKIKISHIA ULIMWENGU KWA HABARI YA HAKI: – Ni kazi ya Roho Mtakatifu kumhakikishia kila tunayemhubiri kwamba Yesu Kristo pekee ndiye mwenye haki na tunahesabiwa haki kwa kumwamini Yeye tu (1 YOHANA 2:1).  Roho Mtakatifu akitenda kazi hii humfanya mtu akiri kwamba Yesu ndiye mwenye haki, kama ilivyokuwa kwa akida katika LUKA 23:47.  Vivyo hivyo, Roho Mtakatifu huwahakikishia watu tunaowahubiria kwamba maneno yale tunayoyasema ndiyo ya haki, na kweli., kuliko yale waliyojifunza katika dini zao.  Tukiwa na Roho Mtakatifu, hatuna haja ya kutumia Misahafu ya dini nyingine kuwahakikishia watu tunavyowahubiri.  Kufanya hivyo, ni ubatili, maana ni kuvithibitisha vitabu hivyo kwamba vina ukweli, na hilo haliwezi kuleta matokeo.
  1. KUUHAKIKISHIA ULIMWENGU KWA HABARI YA HUKUMU: – Watu wengi wenye dhambi, hawaamini kwamba kuna hukumu ya kutupwa motoni baada ya kufa, na kuona kama ni mbinu za kuwaanya waache starehe za dunia.  Watu wengi pia hawaamini kwamba wanaweza kusamehewa dhambi zao kabisa na kufutiwa hukumu, na hudhani kwamba hata wafanyeje kama wameandikiwa motoni basi.  Kazi ya roho Mtakatifu, ni kumhakikishia mtu tunayemhubiria kwamba ni kweli kuna hukumu baada ya kufa na Mhukumu wa Ulimwengu huu ni Yesu.  Vilevile humhakikishia kwamba Mkuu wa Ulimwengu Shetani, yeye amekwisha kuhukumiwa kutupwa katika moto wa milele, na hana nafasi ya kusamehewa, laki8ni sisi tuna nafasi ya kufutiwa hukumu tukimwamini Yesu (WAEBRANIA 9:27; MATHAYO 25:41; YOHANA 3:18, 36).  Kwa msaada wa Roho Mtakatifu ndipo mtu anapoweza kusema kama mhalifu msalabani katika LUKA 23:39-42.

  1. KUWAONGOZA WATU NA KUWATIA KWENYE KWELI YOTE: – Roho Mtakatifu, huwaongoza watu na kuwaonyesha njia ya kweli.  Anaweza hata kusema na watu kwa njia ya ndoto kama mkewe Pilato (MATHAYO 27:19), na kuwaelekeza waende kusali Kanisa fulani, waende katika mkutano fulani wa Injili n.k.  Roho Mtakatifu huwapeleka watu kwenye kweli.  Ndiyo maana tukiwa hatuhubiri kweli katika makanisa yetu, tutaona watu wengi wanachomoka na kuhama wakiongozwa na Roho Mtakatifu kwenye kweli yote, na kwa kukosa ufahamu, tutalalamika kwemba watu wetu WANAIBIWA!  Roho Mtakatifu hawaibi!  Ni watu wake!  Roho Mtakatifu huwaongoza watu kwa wingu na moto (HESABU 9:15-23).  Tabia za Roho Mtakatifu, ni pamoja na hizi zifuatazo tunazojifunza katika mistari hii:
  1. HANENI KWA SHAURI LAKE MWENYEWE: – Maneno ya Roho Mtakatifu SIKU ZOTE hufanana na maneno ya Yesu, hayatofautiani kamwe maana Roho Mtakatifu hutwaa katika yaliyo ya Yesu na kutupasha habari (MST. 13-15).  Yeye ni roho wa kweli, na Yesu ndiye Kweli, hivyo ni sawa pia kusema Yeye ni Roho wa Yesu (MATENDO 16:7).  Roho Mtakatifu, hushuhudia pamoja na Baba na Mwana (1 YOHANA 5:8).  Hivyo mtu akisema ameongozwa na Roho Mtakatifu kumwacha mkewe na kumwoa mke mwingine, ni dhahiri kwamba huyo siyo Roho Mtakatifu, maana Yesu alisema amwachaye mkewe na kumwo mwingine azini, na Baba anachukia kuachana (LUKA 16:18; MALAKI 2:15-16).  Ujumbe au unabii wowote unaodaiwa kwamba unatokana na Roho Mtakatifu, kwa msingi huu, lazima tuupime kwa Neno la Mungu.
  2. NI ROHO WA KWELI: – Hasemi uongo, hivyo ujumbe unaotokana na Roho Mtakatifu unaotupasha habari ya mambo yajayo, hauna budi kutimia.  Hata hivyo, hata ukitimia, lakini unatutoa mbali na kweli ya Neno la Mungu, tujue pia siyo wa Roho Mtakatifu (KUMBUKUMBU 13:1-4).  Inatupasa kuwa waangalifu nyakati za leo kuweka mawazo yetu katika unabii, Roho hutumia njia hii leo mara chache sana, maana anasema nasi leo katika Neno la Mwana wa Mungu Yesu (WAEBRANIA 1:1-2).  Katika Matendo ya Mitume,
tunaona jumbe chache sana za Roho Mtakatifu kwa miaka mingi!

Hata kama tunafahamu mafundisho mengi, hatuna budi kuwafundisha watoto wachanga kiroho hatua kwa hatua, tukiwapa maziwa kwanza.  Tukianza tu kuwafundisha mafundisho magumu mwanzoni, hawawezi kuyastahimili.  Hatuna budi kuwaongoza polepole, tukiwaharakisha watakufa kiroho (MWANZO 33:12-14; 1 PETRO 2:2).

(4)         HUZUNI KUGEUKA KUWA FURAHA 
Matatizo na dhiki tulizo nazo duniani leo, zinafananishwa na uchungu wa uzazi hasa ule wa mtoto wa kwanza (YEREMIA 4:31; 6:24).  Wanafusnzi wa Yesu waliona huzuni Yesu kuwaacha kumbe ilikuwa furaha kwao maana ndipo Roho Mtakatifu anagekuja kwao.  Alipokuja Roho kwao, walifurahi na kusahau huzuni yao (MATENDO 13:52).  Leo tunaweza kuwa na huzuni wakati wa ugonjwa utakaotuuua, lakini tukifa, tutasahu uchungu wote, ikiwa tutakufa tukiwa tumeokoka.  Mateso na dhihaka za waume, wazazi, kukosa hiki au kile kwa ajili ya wokovu, yote haya ni utungu ambao utatuletea furaha kama ya kujifungua mtoto, tutakapomwona Yesu.

Ni sifa ipi ya kutuwezesha kuingia mbinguni?  Ni utakatifu (WAEBRANIA 12:14).  Ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge (UFUNUO WA YOHANA 21:27).  Kinyonge ni kipi?  Ni yule anayetenda dhambi.  Huyu ni mtu asiyefaa, ni mnyonge!  Je, wewe ni mtakatifu?  Jibu ni la!  Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini; hivyo wewe pia ni mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13;  YOHANA 14:6).  Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii?  Najua uko tayari.  Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni;  Mungu Baba asante kwa ujumbe huu.  Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dha 1.MAVAZITUVAAYO YANA UTUKUFU KWA MUNGU WETU
        
SOMO: MASHARTI YA KUMFUATA YESU (MATHAYO 16:21-28)
Katika MATHAYO 16:21-28, kuna mengi ya kujifunza kwa mwanafunzi wa Biblia. Ingawa kichwa cha somo letu ni “MASHARTI YA KUMFUATA YESU”, ni muhimu kufahamu kwamba hiki ni kipengele kimoja tu katika vipengele vinne vinavyotuongoza katika kuyatafakari yote tunayoyapata katika mistari hii. Vipengele hivi vinne vya somo letu la leo, ni hivi vifuatavyo:-
(1) KUTABIRIWA KWA KIFO NA KUFUFUKA KWA YESU (Mst. 21);
(2) KUSHAWISHIWA KWENDA MBALI NA MPANGO WA MUNGU (Mst. 22-23);
(3) MASHARTI YA KUMFUATA YESU (Mst. 24-26);
(4) KUTABIRIWA KWA KUJA KWA YESU MARA YA PILI (Mst. 27-28).
(1) KUTABIRIWA KWA KIFO NA KUFUFUKA KWA YESU (Mst. 21)
Kifo cha Yesu Kristo hakikuwa kifo cha kawaida. Yesu Kristo hakukutwa na kifo chake bila kufahamu mapema kama wanadamu wengine. Mapema sana, Yesu Kristo, alitabiri na kufundisha jinsi atakavyokufa na kwamba atafufuka siku ya tatu. Alirudia mara kwa mara kueleza hivyo (MATHAYO 17:22; 20:17-19; 26:1-2; MARKO 8:31; 9:31; 10:32-34; LUKA 9:22,44; 18:31-34). Ilikuwa ni mpango wa Mungu, Yesu Kristo kufa. Alikuja duniani ili afe kwa sababu zifuatazo:-
1. Awe ni mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu (YOHANA 1:29; 1 WAKORINTHO 5:7; 1 PETRO 1:19; ISAYA 53:7; 1 YOHANA 3:5; WAGALATIA 1:4);
2. Afe kwa niaba yetu, achukue adhabu yetu ya mauti ya milele (WAEBRANIA 2:9; WAGALATIA 3:13; 1 PETRO 3:18).
Kufufuka kwake kulionyesha ushindi juu ya mauti. Sisi nasi kwa kumwamini tunapewa kushinda uchungu wa mauti yaani dhambi (1 WAKORINTHO 15:56-57).
(2) KUSHAWISHIWA KWENDA MBALI NA MPANGO WA MUNGU (Mst. 22-23)
Tunapodhamiria kutekeleza mpango wowote wa Mungu kwetu, ni muhimu kufahamu kwamba watakuwepo watu watakaotumiwa na Shetani kutushawishi kuuacha mpango wa Mungu kwetu. Watu hawa watakuwa watu wa nyumbani kwetu yaani ndugu zetu wa kimwili na kiroho walio karibu nasi. Watatumia maneno ya kutuonea huruma kwa yale yatakayotugharimu au kutupata katika kutekeleza mpango huo. Hatupaswi kuwasikiliza. Siyo wao ila ni shetani anayewatumia. Kazi yetu ni kumtii Mungu na kumpinga Shetani naye atatukimbia (YAKOBO 4:7).
MASHARTI YA KUMFUATA YESU (Mst. 24-26)
1. KUJIKANA MWENYEWE KILA SIKU – Kuyaacha mapenzi yetu, furaha zetu na matakwa ya miili yetu yaliyo kinyume na Mungu. Kukataa uhuru wowote ulio mbali na haki na kutafuta kila siku uhuru ulio mbali na dhambi (WARUMI 6:20-22; 8:12-13);
2. KUJITWIKA MSALABA – Tunapaswa kujitwika msalaba kila siku katika kumfuata Yesu (LUKA 9:23). Msalaba ni dalili ya aibu, kudharauliwa, kudhihakiwa, kulaumiwa, kutukanwa na pia kupata maudhi na mateso. Kila siku lazima tukubali kuyabeba haya na kudumu tu katika imani (2 TIMOTHEO 3:12; WAFILIPI 1:29-30; WAKOLOSAI 1:23).
3. KUMFUATA YESU KILA SIKU – Ili tukae na Yesu milele, tunapaswa kumfuata Yesu kila siku, saa na dakika; siyo kwa muda fulani tu wakati wa raha, mahitaji n.k. (YOHANA 10:27).
(4) KUTABIRIWA KWA KUJA YESU MARA YA PILI (Mst. 27-28)
Kama Yesu alivyotabiri kufa na kufufuka kwake na ikatokea vivyo hivyo, ni muhimu kufahamu pia utabiri huu utatimia wakati wowote ujao. Ni muhimu kuifanya kazi ya Mungu kwa bidii ili tulipwe kadri ya matendo yetu (1 WAKORINTHO 15:58; UFUNUO 14:13).
Katika Mst. 28, wanafunzi wanaotajwa kwamba hawataonja mauti mpaka wamemwona Yesu akija katika Ufalme wake, ni Petro, Yakobo na Yohana ambao walipelekwa juu ya mlima mrefu faraghani na huko wakamwona Yesu katika utukufu wa Ufalme wake (MATHAYO 17:1-2).
……………………………………………………………………..
Mpendwa msomaji, unaona sasa! Hakuna haja ya kusema, “Hivi kweli nitaweza kushinda dhambi duniani? Hivi kweli maisha ya wokovu nitayaweza?” Ni Neema juu ya Neema. Unalotakiwa kufanya ni kutubu dhambi zako tu kwa kumaanisha kuziacha; kwa imani tu, na mengine yanayofuata mwachie Yesu; na leo hii utashangaa kuona maisha yako yamebadilika ghafla na kwa urahisi utaona unaweza kufanya mapenzi ya Mungu, bila jitihada za kibinadamu. Je, uko tayari kutubu dhambi zako? Najua uko tayari. Basi sema hivi, “Mungu wangu, natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha kuanzia leo. Asante kwa neema yako ambayo kwa hiyo tunaokolewa kutokana na kazi aliyoifanya Yesu. Niokoe sasa na kunipa neema ya kufanya mapenzi yako kuanzia sasa na wakati wote ujao. Asante kwa kuniokoa katika Jina la Yesu. Amen”. Ili uzidi kuukulia wokovu ulioupokea leo, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu. MUNGU AKUBARIKI !!!

JINA LA YESU KRISTO – MOJAWAPO YA FUNGUO ZA UFALME WA MBINGUNI

“Nami nakuambia ….. na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lolote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lolote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni” (Mathayo 16:18 – 19).
Maneno haya ya Yesu Kristo yanatuonyesha kuwa, nia yake ni kulijenga kanisa lililo na mamlaka kuliko shetani. Kanisa ni mwili wake (Waefeso 1:22 – 23). Wakristo waliookolewa kwa damu ya Yesu Kristo ni viungo vya mwili wa Kristo – ni viungo vya kanisa (1 Wakorintho 12:12, 13, 27). Kwa hiyo Yesu Kristo anaposema atalijenga kanisa lake wala milango ya kuzimu haitalishinda – ana maana ya kuwa, kila mkristo aliye wake anajengwa kiroho awe na mamlaka ya kumshinda shetani.
Ni budi tufahamu ya kuwa, Yesu Kristo hawezi kutuambia tufungue kama hakuna kitu cha kukifungua. Hawezi kutuambia tufunge kama hakuna kitu cha kufunga. Kwa hiyo ni lazima kuna vitu vya kuvifunga na kuna vitu vya kuvifungua.
Pia, tufahamu ya kuwa, Yesu Kristo hawezi kutuambia tufunge na kufungua kabla hajatupa uwezo na mamlaka ya kufanya hivyo. Uwezo na mamlaka tunapata ndani ya Kristo aliyetukabidhi funguo za ufalme wa mbinguni.
Itakuwa haina maana kwa Yesu Kristo kutukabidhi funguo bila ya kutufundisha namna ya kuzitumia. Hawezi kutukabidhi mamlaka bila kutufundisha namna ya kuyatumia.
Yesu Kristo anasema tukifunga au tukifungua, mbinguni nako kunatia mhuri kitendo hicho. Hatuwezi kufanya hivyo kama tulichokifanya hakifanani na mapenzi yake. Ndiyo maana tunaomba kuwa mapenzi yake yatimizwe hapa duniani, kama yanavyotimizwa huko mbinguni. Kwa maneno mengine tunaweza kusema ya kuwa ukifanya kitu chochote katika mapenzi ya Mungu, Ufalme wa mbinguni utakuwa upande wako.
Aina za Funguo:
Biblia inazungumza juu ya funguo za aina tano zifuatazo:
Funguo za Ufalme wa Mbinguni – Mathayo 16:19 – Yesu Kristo amekabidhi funguo hizi kwa wakristo (Kanisa).
Funguo za mauti na za kuzimu – Ufunuo 1:18 – Funguo hizi anazo Yesu Kristo – baadaye atampa Malaika mmoja funguo za kuzimu ili amfunge Ibilisi (Ufunuo 20:1-3).
Ufunguo wa nyumba ya Daudi – Isaya 22:22; Ufunuo 3:7. Ufunguo huu anao Yesu Kristo.
Ufunguo wa kawaida wa mlango – Waamuzi 3:25.
Neno ‘funguo’ lililoandikwa katika Mathayo 16:19; Ufunuo 1:18; Isaya 22:22 na Ufunuo 3 – 7 lina maana ya ‘mamlaka’. Kazi ya funguo ni kufunga na kufungua. Kwa hiyo ukipewa funguo maana yake umepewa mmalaka ya kufunga na kufungua.
Kwa mfano, mtu akikupa funguo za chumba – maana yake una mamlaka juu ya chumba hicho kukifunga na kukifungua. Mtu yeyote akitaka kuingia kwenye chumba hicho hawezi kufanya hivyo bila kupata ruhusa toka kwako ya kumfungulia. Ukipewa funguo za gari maana yake kwa muda huo ambao una funguo hizo za gari, una ‘mamlaka’ juu ya hilo gari kulifunga lisitumike au kulifungua litumike. Mtu akitaka kulitumia ni budi aje kwako kwa ajili ya kufuata funguo.
Kwa hiyo Yesu Kristo aliposema ametupa funguo za ufalme wa mbinguni alikuwa ana maana ya kuwa ametupa ‘mamlaka’ ya ufalme wa mbinguni. Ni vizuri ufahamu hapa ya kuwa ufalme wa mbinguni ni ufalme wa Mungu ulio na mamlaka juu ya falme nyingine zote – ufalme wa shetani, ufalme wa wanyama, ufalme wa wadudu, ufalme wa mimea, ufalme wa ndege, na kadhalika. Ikiwa wewe ni mkristo uliyeokoka basi fahamu ya kuwa, una mamlaka uliyopewa na Yesu Kristo juu ya falme hizi zote!
Yesu Kristo anaendelea kusema kuwa; lolote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lolote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.
Kwa mfano ukiamua kumfunga ibilisi asikusumbue katika maisha yako, mbinguni pia wanasimamia utekelezaje wa jambo hili. Hata kama ibilisi ataamua ‘kukata rufaa’ juu ya uamuzi wa kumzuia asikusumbue na akaenda kwa Mungu kuomba aachiliwe – Mungu atamwambia ‘rudi kwa aliyekufunga, akikufungua nami nitakufungua, lakini asipokufungua nami sikufungui’
Unaweza kusema mbona shetani alipewa ruhusa na Mungu kumjaribu Ayubu. Kumbuka kuwa Ayubu aliishi katika agano la kale na sisi tunaishi katika agano jipya ambalo ndani yake tuna mamlaka ya kumfunga shetani kwa jina la Yesu Kristo.
Kuna wakristo wengi wameonewa na ibilisi kwa kuwa hawajui mamlaka waliyo nayo na namna ya kuyatumia.
Jambo jingine ninalotaka uone hapa ni kwamba Yesu Kristo alisema ametupa “funguo ZA ufalme wa mbinguni”; na hakusema ametupa ufunguo wa ufalme wa mbinguni.
Neno hili ‘ZA’ lina maana ya kuwa kuna funguo za ufalme wa mbinguni zaidi ya mmoja. Kumbuka kuwa kuna tofauti ya funguo za ufalme wa mbinguni na zile funguo za mauti na za kuzimu
Funguo za mauti na za kuzimu alikuwa nazo shetani hadi aliponyang’anywa funguo hizo na Yesu Kristo kwa kufa kwake msalabani na kufufuka. Funguo za mauti na za kuzimu anazo Yesu Kristo sasa.
Funguo za ufalme wa mbinguni anazo Yesu Kristo, lakini amezikabidhi kwa wakristo waliomo duniani wazitumie.
Ukifuatilia maneno yaliyomo katika agano jipya utaona ya kuwa kuna funguo NNE za ufalme wa mbinguni nazo ni:
1. Jina la Yesu Kristo
2. Damu ya Yesu Kristo
3. Neno la Yesu Kristo
4. Nguvu za Roho Mtakatifu
Katika somo hili tunajifunza juu ya jina la Yesu Kristo ambalo ni mojawapo ya funguo za ufalme wa mbinguni.
Tumia mamlaka uliyopewa:
Kuna wakati fulani ambapo nilihangaika siku nyingi kwa kuomba na kwa kulia usiku na mchana ili shida niliyokuwa nayo iniondoke bila mafanikio. Nilikuwa naomba kwa Mungu, lakini sikuona mabadiliko yoyote, ilikuwa kama vile Mungu ameziba masikio yake asisikie maombi yangu. Pamoja na maombi niliongeza kulia zaidi lakini sikufanikiwa pia.
Nikiwa katika hali ya kukata tamaa huku nikijiuliza kwa nini naomba kwa Mungu lakini shida inayonisumbua haiondoki – Roho Mtakatifu alisema ndani ya roho yangu maneno haya; “shida yako inayokusumbua imeletwa na shetani. Unayo mamlaka ya kumkemea shetani naye ataondoka na shida uliyonayo itakwisha. Kama hufahamu juu ya mamlaka uliyonayo soma vitabu vya Waefeso, Wafilipi, Wakolosai na vitabu vingine katika Biblia”
Niliposikia maneno hayo nikaomba tena; “Ee Bwana nifundishe juu ya mamlaka uliyonipa ili nipate kuyatumia.”
Namshukuru Mungu ya kuwa alisikia sala yangu na alianza kunifundisha juu ya mamlaka aliyonipa, na bado anaendelea kunifundisha hatua kwa hatua kila siku.
Nilipoendelea kujifunza ndipo nilipotambua kuwa si kila shida uliyonayo itaondoka kwa maombi – bali shida nyingine zinaondoka kwa KUAMURU katika jina la Yesu Kristo shida hiyo iondoke au kwa KUAMURU hali unayoitaka itokee.
Kwa hiyo siku moja usiku niliamua kutumia mamlaka niliyonayo katika jina la Yesu Kristo shetani aondoke katika eneo alilokuwa ananiletea shida – mara hiyo hiyo kulitokea mabadiliko. Shida iliyonisumbua kwa muda mrefu ilitoweka mara moja. Badala ya kusubiri Mungu afanye kitu kwanza juu ya shida hiyo, niliamuru iondoke na Mungu akasimamia utekelezaji wake!
Ndivyo alivyomaanisha aliposema “Lolote utakalolifunga (wewe!) duniani, litakuwa limefungwa mbinguni” – Maana yake Mungu atausimamia uamuzi wako wa kulifunga hili jambo! Ukiamua kulifunga, Mungu atalifunga pia! Anayeanza kufanya kitu ni wewe!
Hivi ndivyo Mtume Petro alivyofanya alipomkuta yule mtu aliyekuwa kiwete tangu tumboni mwa mama yake – wakati huo alikuwa ana umri usiopungua miaka arobaini akiomba sadaka katika mlango wa kuingia hekaluni.
Mtume Petro alipomwona hakumwomba Mungu amponye bali alimwamuru asimame na kutembea kwa Jina la Yesu Kristo! Alisema hivi; “Kwa Jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende”. Halafu; “Akamshika mkono wa kuume, akamwinua, mara nyayo zake na vifundo vya miguu yake vikatiwa nguvu. (Yule aliyekuwa kilema) Akaondoka upesi akasimama, akaanza kwenda, akaingia ndani ya hekalu pamoja nao, akienda, akirukaruka, na kumsifu Mungu” (Matendo ya Mitume 3:6 – 8).
Kile alichoamuru Mtume Petro kitokee kwa jina la Yesu Kristo kilitokea. Alimwamuru yule kilema asimame na kutembea kwa jina la Yesu Kristo na ikawa hivyo!
Na wewe unaweza kufanya hivyo ikatokea! Kwa nini? Kwa sababu na wewe umepewa jina la Yesu Kristo lenye uwezo usiobadilika! Kumbuka Yesu Kristo alisema hivi;
“Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; Kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya” (Marko 16:17-18).
Labda umeyasoma maneno haya mara nyingi kiasi kwamba umeyazoea, na yameanza kupoteza uzito wake. Ni maombi yangu kwa Mungu kuwa Roho Mtakatifu ayahuishe upya maneno haya ndani yako ili uyaone kama Yeye anavyotaka uyaone.
Siku moja nilikuwa nafundisha neno la Mungu mahali fulani, na baada ya mafundisho alijitokeza mtu mmoja aliyesema anaumwa kifua na kwamba aliihitaji aombewe.
Nilimwambia aweke mkono wake kifuani mahali alipokuwa anaumwa – na akafanya hivyo. Na mimi nikaweka mkono wangu juu ya mkono wake uliokuwa kifuani pake, halafu nikasema “Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti”! Nilipotamka tu jina hili la ajabu, yule mtu akaanguka chini na majini yaliyokuwa yanabana kifua chake na kuleta maumivu yalianza kupiga kelele. Nikayaamuru yamtoke mtu huyo kwa jina la Yesu Kristo – na yakamtoka wakati huo huo – mtu huyo akasimama akiwa mzima!
Kwa nini ilikuwa hivyo? Kwa kuwa Yesu Kristo alisema kwa jina lake tutatoa pepo! Na ndivyo ilivyo! Tumia mamlaka uliyo nayo usiogope! Ikiwa wewe ni mwamini yaani umeokoka, jina la Yesu Kristo ni lako – ni uamuzi wako kulitumia au kutokulitumia.
Siku nyingine niliitwa kwenda kumwombea mama mmoja ambaye alikuwa hawezi kuinuka kitandani kwa muda wa miezi miwili kwa sababu ya ugonjwa wa homa. Nilipofika katika nyumba hiyo niliweka mkono wangu juu ya kichwa cha mama yule na kuiamuru homa imwache kwa jina la Yesu Kristo, kisha nikaondoka. Nilimwacha yule mama akiwa amelala. Kesho yake mtoto alikuja kuniambia kuwa mama yake amepona, ameamka toka kitandani na anafanya kazi! Jina la Yesu Kristo libarikiwe milele.
Yesu Kristo alisema tukiweka mikono yetu juu ya wagonjwa kwa jina lake, watapata afya. Na ndivyo inavyotokea tukitii agizo hili. Kuna uweza usiopimika katika jina la Yesu Kristo. Ni ufunguo unaowafungua watu toka katika minyororo ya shetani. Usiogope. Uwe na moyo wa ushujaa na ujasiri mwingi – tumia mamlaka uliyonayo katika jina la Yesu Kristo.

JINSI YA KUSIFU

ZABURI: Enyi watu wote pigeni makofi, mwimbieni Bwana.kwa kuwa bwana aliye juu ni mfalme wa yote atawatiisha mataifa chini ya miguu yetu.
Sababu za kumsifu Mungu:
1. Tunamsifu kwa vile alivyo. Ametukuka sana, ana nguvu.
2. Tunamsifu mungu kwa sababu ya matendo yake makuu.
Biblia katika Zaburi inasema Kwa kuwa Mungu ni mfalme mwimbieni kwa Akili, Paulo anasema imetupasa kuomba kwa Roho na kwa Akili pia. Nyimbo zinazotakiwa wakati wa sifa ni zile ambazo zinamsifu Mungu tu, na sio zilizokaa kama mipasho.
Pambio kama hizi za mipasho sio za sifa, pambio za sifa ni zile ambazo tunakuwa tukiimba kumsifu mungu, tukitaja sifa zake kama Ukuu wake, Uweza wake.
Kunatofauti katika Kuabudu na sifa isipokuwa zinashabiriana.
Kuabudu maana yake ni kuinama na kusujudu na kutukuza kitu kuwa hiki ni kikuu kuliko chochote, wimbo wa kuabudu sio lazima uwe wa taratibu.
Kuabudu ni kuinama na kumuinua Mungu. Zamani tulipokuwa tunaabudu tulikuwa tunanyoosha kabisa mikono, lakini siku hizi tunainua kwa imani tu .
Biblia inasema Maana Mungu ni mfalme inawapasa kumuimbia kwa akili: mambo haya hayatatimia kama hatufuati utaratibu ulio sahihi.
mbi.  Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha.  Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo.  Bwana Yesu niwezeshe.  Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu.  Amen.  Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni.  Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.  MUNGU AKUBARIKI !!!

  1. tunaowahubiria kwamba maneno yale tunayoyasema ndiyo ya haki, na kweli., kuliko yale waliyojifunza katika dini zao.  Tukiwa na Roho Mtakatifu, hatuna haja ya kutumia Misahafu ya dini nyingine kuwahakikishia watu tunavyowahubiri.  Kufanya hivyo, ni ubatili, maana ni kuvithibitisha vitabu hivyo kwamba vina ukweli, na hilo haliwezi kuleta matokeo.

tofauti na jinsi alivyokuwa mwanzo kabla hajaokolewa (MATHAYO 5:16; 2WAKORINTHO 3:2-3).

No comments:

Post a Comment