Namshukuru mwenyezi MUNGU ALIYENIPA uhai tena nikitambua ni kwa neema tu peke yangu sikustahili .Lakini kwasababu ya rehema zake na ukuu wa peke yake ahimidiweISAYA66:1-4;1 Bwana asema hivi, Mbingu ni kiti changu cha enzi, na dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu; 2..... .NA TUMUOMBE KWA BIDII KWA SABABU NI AHADI YAKE .isaya 55;6-12 Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu; 7........
Friday, 20 June 2014
Wednesday, 18 June 2014
TUJIFUNZE MAANDIKO

A.MAVAZI YA KIDUNIA
MITHALI 7:10
“Na tazama, mwanamke akamkuta ana mavazi ya kikahaba”. Kwa muda mrefu, katika kanisa la Mungu duniani, wakristo wengi wamegubikwa na utata mwingi kuhusiana na somo la mavazi. Maswali yafuatayo yamekuwa yakiulizwa bila kupata majibu sahihi:-
Je, mkristo anaweza kuvaa vazi lolote alipendalo?
Je, Mungu anaangalia moyo tu na haangalii mambo ya nje kama mavazi?
Katika somo hili la mavazi ya kikahaba lililojaa wingi wa mafunuo ya kipekee, unaweza kupata majibu ya maswali haya na mengi mengine; kwa kina, mapana, marefu, kwa ufasaha mkubwa. Katika somo hili utapata maarifa ambayo kila mtu anayeokolewa anapaswa ayapate katika uchanga wake wa kiroho ili aweze kuwa tofauti na watu wa dunia (mataifa). Ili aweze kuwa nuru au barua inayosomeka vizuri : 1.MAVAZITUVAAYO YANA UTUKUFU KWA MUNGU WETU
A.MAVAZI YA KIDUNIA
MITHALI 7:10
“Na tazama, mwanamke akamkuta ana mavazi ya kikahaba”. Kwa muda mrefu, katika kanisa la Mungu duniani, wakristo wengi wamegubikwa na utata mwingi kuhusiana na somo la mavazi. Maswali yafuatayo yamekuwa yakiulizwa bila kupata majibu sahihi:-
Je, mkristo anaweza kuvaa vazi lolote alipendalo?
Je, Mungu anaangalia moyo tu na haangalii mambo ya nje kama mavazi?
Katika somo hili la mavazi ya kikahaba lililojaa wingi wa mafunuo ya kipekee, unaweza kupata majibu ya maswali haya na mengi mengine; kwa kina, mapana, marefu, kwa ufasaha mkubwa. Katika somo hili utapata maarifa ambayo kila mtu anayeokolewa anapaswa ayapate katika uchanga wake wa kiroho ili aweze kuwa tofauti na watu wa dunia (mataifa). Ili aweze kuwa nuru au barua inayosomeka vizuri tofauti na jinsi alivyokuwa mwanzo kabla hajaokolewa (MATHAYO 5:16; 2WAKORINTHO 3:2-3).
Siku hizi za mwisho, tumekuwa na walimu wengi katika kanisa la Mungu ambao hufundisha kuwa Mkristo anaweza kuvaa vyovyote vile kwa hoja mbalimbali. Kabla hatujaziangalia hoja zao, hatuna budi kufahamu hili kwanza. Mungu ametahadharisha juu ya kuwepo kwa walimu wengi wa uongo. Kumbuka neno WENGI (2 PETRO 2:1-3; MATHAYO 24:11). Hukumu ya walimu wa uongo itakuwa kubwa sana ( YAKOBO 3:1). Hatuna budi kujua kuwa wote tutahukumiwa sawasawa na injili ya Paulo mtume (WARUMI 2;16). Paulo mtume anasema, injli inayohubiriwa kinyume na injili yake ni injli ya namna nyingine (WAGALATIA 1:6-9). Yeyote anayehubiri injili kinyume na injili ya Paulo mtume amelaaniwa na hawezi kuingia mbinguni (MATHAYO 25:41).Tukijua kuwa tumezungukwa na upepo wa elimu ya uongo (WAEFESO 4:14), tunapaswa kuchunguza maandiko kwa umakini. Watu wa Beroya, waliyachunguza maandiko kuona kama ndivyo yalivyo wakati Paulo na Sila walipokuwa wakiwafundisha (MATENDO 17:10-11). Maana hatuwezi kutenda neno lolote kinyume cha kweli, bali kwa ajili ya kweli (2WAKORINTHO 13:8). Kweli ni Neno la Mungu (YOHANA 17;17). Zifuatazo ni hoja za baadhi ya walimu wanaofundisha Neno la Mungu:-
HOJA YA KWANZA
Mungu haangalii mambo ya nje, anaangalia mambo ya ndani. Wanafundisha wakisema mavazi hayawezi kumzuia mtu kuingia mbanguni. Wanawatia moyo watu waendelee kuvaa mavazi wapendavyo bila kuangalia maandiko yanavyosema
Tunapaswa kujua kuwa utakatifu ni mwili na roho siyo ndani tu kama wao wasemavyo (1 WAKORINTHO 7:34; 2 WAKORINTHO7:1; 1WATHESALONIKE 5:23). Bwana Yesu alifundisha juu ya utakatifu kwamba unaanzia ndani na kasha nje. Hapo ndipo tunakuwa tumeutimizav utakatifu mwili na roho (MATHAYO 23:25-26). Yesu alisema “tutawatambua kwa matunda yao” (MATHAYO 7:15-21).Mtihutambulika kwa matunda yake. Matunda hayakai ndani ya mti, huwa nje ya mti. Hivyo, mavazi yanaweza kumtambulisha mtu, yeye ni nani na kazi yake ni ipi. Hata kwa kahaba ni hivyo (MITHALI 7:10).
HOJA YA PILI
Tuko huru ndani ya Yesu. Palipo na roho wa Mungu ndipo penye uhuru (WAGALATIA 5:1; 2WAKORINTHO 3;17). Hatuna budi kujua, kabla hatujaokolewa tulikuwa watumwa (YOHANA 8:33-36). Anachozungumzia Yesu ni uhuru mbali na dhambi (WARUMI 6:16-18). Baada ya kuokolewa sisi tunakuwa watumwa wa haki. Kwa hiyo, uhuru unaozungumziwa siyo wa kuvaa chochote au wa kufanya chochote kinyume cha Neno la Mungu.
HOJA YA TATU
Hatuko chini ya sheria wakati huu wa neema. Hatuna budi kufahamu kuwa, dhambi ni uasi wa sheria. Bila kuiasi sheria wewe si mwenye dhambi(1 YOHANA 3:4). Walimu hao, hutumia maandiko haya (WAGALATIA 5:4-5; ; WARUMI 6:14; WAGALATIA 5:18). Tunapaswa kufahamu kuwa, tumeokolewa na kutoka katika sheria ya Musa (WAEBRANIA 10:28). Hii ndio huitwa kongwa la utumwa. Tumetolewa kuwa chini ya sheria ya Musa na kuwekwa chini ya sheria ya Kristo (WAGALATIA 6:2). Sharia ya Kristo ni ngumu kuliko sheria ya Musa (MATHAYO 5:27-44). Sheria ya Yesu ni sheria ya Kifalme (YAKOBO 2:8). Sheria ya kifalme siyo ya kuchezea. Mfalme akiagiza jambo hana mjadala.
HOJA YA NNE
Tuvae vyovyote ili tuwapate na mataifa. Walimu hao wanaamua kushusha viwango na kujaribu kurahisisha njia ya kwenda mbinguni(1 WAKORINTHO 3:11). Msingi umekwisha kuwekwa ambao ni Yesu Kristo. Yesu ni mchungaji mkuu, wachungaji wote wako chini ya mchungaji huyo. Wachungaji wanapaswa kujifunza kwa mchungaji mkuu Yesu Kristo (WAEBRANIA 13:20). Alionesha kielelezo kwa kutokushusha viwangop vya mafundisho ili kuwa na idadi kubwa ya washirika (YOHANA 6:61, 66-68). Wengi miongoni mwa wanafunzi wake walirejea nyuma na wasiambatane naye ( Yesu ) tena. Kilichowafanya kukwazika ni mafundisho magumu kutendea kazi ( Neno gumu ). Yesu kristo ili kuonesha mfano kwa wachungaji wa sasa, yeye hakuchuja Neno lake ili waendelee kuwepo bali hata wale wachache (tenashara/mitume) aliwageukia na kuwauliza kama na wao wanataka kuondoka..Alikuwa tayari kubaki peke yake na kuanza kazi upya. Tunaweza kuwa na orodha ndefu ya majina ya washirika waliojiandikisha kanisani lakini majina hayo yakawa hayapo katika kitabu cha majina ya Mungu (kitabu cha uzima). Hatuwezi kuwaingiza watu mbinguni kwa viwango vyetu wenyewe, ni kwa kuongozwa na Neno la Mungu tu.
Wakitoka ndipo tunapojua kuwa hawakuwa wa kwetun(1 YOHANA 2:19). Sharti kanisa liongezeke kwa watu wanaookolewa na si vinginevyo (MATENDO 2:47). Mtu aliyeokolewa, amri za Mungu siyo nzito kwake (1YOHANA 5:1-5). Tunapaswa kujua kuwa watakaoingia mbinguni hawatakuwa wengi ukilinganisha na watakaotupwa motoni (MATHAYO 7: 13-14). Mataifa watutambua kuwa tumeokoka kwa matendo yetu (1 PETRO 2:12; 2WAKORINTHO 3:1-3; MATHAYO 26:69-73).
MAJUM
Ujira au mshahara wa kahaba na hanithi hautakiwi kupokewa ndani ya nyumba ya Mungu (Torati 23:17-18). Kama biblia inataja juu ya kuwepo kwa mavazi ya kikahaba, hatutakiwi kupuuzia.. Mtu akiokoka anapaswa kubadilika kwa kuyafanya matendo yanayoambatana na kutubu kwake (MATENDO 26:20). Tunapaswa kuzaa matunda na yaonekane (MATHAYO 3:8). Tukikosa ushuhuda mzuri, tunawafungia wengine kuingia katika ufalme (MATHAYO 23:13). Watu wanaookoka wanatoka katika mazingira na hali tofauti hivyo tunatakiwa kuwafundisha ili waishi sawa na viwango vya Neno la Mungu. Pia desturi na tamaduni zetu zinaweza kuwa kinyume na Neno la Mungu kwa sababu waanzilishi wake wengine hawajaokoka. Neno linasema tusifuate nasaba zisizo na ukomo. Nasaba ina maanisha tamaduni. (1 TIMOTHEO 1:3-4). Mavazi ya kikahaba yanakuwa na lengo la kuwavuta hao tunaotaka kufanya nao uchafu.
Ifuatayo ni misingi inayotupa kujua mavazi ya kikahaba.
- MSINGI WA KWANZA
Mungu anasema katika Neno lake “wala msimpe Ibilisi nafasi” (WAEFESO 4:27). M,apepo yana uwezo wa kufanya uzinzi au uasherati na binadamu. Yanaweza kuja kwa namna mbalimbali (WALAWI 17:7). Waathirika wakubwa wa nguvu za giza (mapepo na majini ) ni wanawake na mgogoro mkubwa ni kwenye mavazi ya kikahaba. Mavazi ya kikahaba ni mlango mkubwa wa mashetani kuwashambulia watu. Kubadili matumizi ya asili ya viungo vya binadamu yawe yasiyo ya asili nyuma yake kuna mashetani. Tukifanya hivyo tutakuwa tunampa nafasi Ibilisi (MWANZO 19:1-28; YUDA 1:6-8). Wakati wa Ruthu katika mji wa Sodoma na Gomora na miji jirani, walifanya uchafu wa kila namna wanaume na wanawake wakiwakiana tama lakini nyuma yake yalikuwepo mashetani (YUDA 1:6-8) “Wakaendelea kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili”. Kumbe kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili nyuma yake kuna mashetani. Kazi ya shetani ni kuharibu mpango wa Mungu wa uumbaji, mpango wa Mungu wa maumbile (YOHANA 10:10). Mtu akipagawa na mashetani ndipo anaanza kuharibu mpango wa Mungu kwa kufanya mambo yasiyo ya asili (MARKO 5:1-20; WARUMI 1:26-28). “Mungu akaona kila alichokifanya (kiumba) na tazama ni chema (kizuri) [MWANZO 1:31]. Shetani anatupandikizia mawazo mabaya tuone kuwa Mungu alikosea katika uumbaji wake. Anatufanya tuone nywele za wazungu ni nzuri sana kuliko zetu waafrika. Pia anatufanya tuone rangi ya ngozi yao ni nzuri kuliko yetu hii nyeusi n.k. Kufanya kinyume na uumbaji wa Mungu wa maumbile yetu ni kumsahihisha Mungu. Kiumbe kinamuona yeye aliyekiumba hana ufahamu. Kitendo hicho ni sawa na kutaka kumpindua Mungu kwenye kiti chake cha enzi. Ni dharau ya hali ya juu (ISAYA 29:16; WARUMI 9:19-21). Ujasiri wa kumdharau Mungu unatoka wapi? Bila shaka unatoka kwa shetani. Mungu anasema “Wao wanaoniheshimu nitawaheshimu na wanaonidharau watahesabiwa kuwa si kitu (1 SAMWELI 2:30).
UHISHO
B.
Subscribe to:
Posts (Atom)