Friday, 13 May 2016

Kazi ya hukumu tumuachie Mungu

Namshukuru mwenyezi Mungu muumba wa nchi na dunia, kwa kibali chake alichonipa. Nani alijua kuwa leo ningekuwa hai! Lkn kwa uwezo wake naishi. Wapendwa leo nataka nizungumze nawe jambo hili; Japo Maandiko matakatifu yameonya sana kuhusu hukumu ya kibinadamu lkn watu/ watumishi wa Mungu tumeweka uzi mnene kwenye mifereji ya masikio yetu ,uku tukiulazimisha ubongo uctunze kumbukumbu ili usahihi wetu katka hili usipotee. Tumekuwa wa kwanza kuoneshea kwa shahada tukisahau mwelekeo wa vidole vinne.Tumekuwa wa kwanza kushabikia kuwa simba ni mnyama hatari na muuaji sana kuliko wanyama wote .Tukisahau kuwa mbu wanongoza safu ya vifo,tumekuwa wa kwanza kusema mtu fulani mdhambi kwa sababu ya uzinzi,wizi au mauaji.tukisahau twaua kwa vinywa,twazini kwa macho na mengine mengi .Yamkini unamdhani katenda dhambi ametubu tayari na na wewe maskini utaoni cha kutubia. Je uoni malali inakupeleka pabaya? cna jibu....................................MUNGU WANGU MBINGUNIV AWABALIKI