Tuesday, 18 November 2014







USIKATE TAMAA MTUMISHI WA MUNGU KWA SABABU YA MAPITO


MTUMISHI WA MUNGU YESU ASIFIWE? (…)”ISAYA40: 27Kwa nini unasema, Ee Yakobo, nanyi Ee Israeli, kulalamika,“Njia yangu imefichwa BWANA asiione,Mungu wangu hajali shauri langu?” 28Je wewe, hufahamu?Je wewe, hujasikia?BWANA ni Mungu wa milele,Muumba wa miisho ya dunia. Hatachoka wala kulegea,wala hakuna hata mmoja awezayekuupima ufahamu wake.”JIBU  YEREMIA32; 27“Mimi ndimi BWANA, Mungu wa wote wenye mwili, Je, kuna jambo lo lote lililo gumu nisiloliweza? NA ISAYA49;15 “Je, mama aweza kumsahau mtoto aliyeko matitini mwake akinyonya?Wala asiwe na huruma juu ya mototo aliyemzaa?Ingawa anaweza kusahau,Mimi sitakusahau wewe!
Namshuru MUNGU ambaye ametupa kusudi na sababu angalau yakusema amina! Kwa sababu sio kwamba ni kwa juhudi au matendo ,lakini neema ambapo tumestahilishwa kuwa tulivyo leo.Mtumishi (watumishi) wa MUNGU leo nataka tuzungumzie dhana ambayo ni ya kawaida sana katika maisha ya kila siku ya watu hasa  wale ambao hawajui maana na malengo ya damu ya yesu msalabani pale alipsema kuwa yote yamekwisha kwa dhamana aliyoitoa kupitia aibu na mateso pale msalabani. Lakini lakushangaza na kushutusha ni kwa wale watumishi wa MUNGU ambao wanatambua hayo yote ila bado wanateteleshwa na kuhuzunishwa na hata mambo madogo ambapo baada ya kuwa mabalozi na kuwatia moyo wale wanaokuwa katka ukristo na wale ambao wako nje wanawakatisha tamaa na kuwavunja moyo kwa kuwaeleza kuwa hawatoweza hata kama wameamua kusonga mbele na pia watu wakulalamika kila iitwayo leo hata kesho pia.LEO tuzungumzie njinsi ya kuudhibitishia ulimwengu kuwa sisi ni wateule pia wana wa Mungu na muda wote kuonekana mashujaa wa kristo wa ukweli.


1.                KUUMIZWA/KUUDHIWA AU KUTESWA NA KUONEWA
Watumishi wa MUNGU pengine tumekuwa watu wa kukata tamaa na pia watu wa kukata shauri za mapema sana hapa bila kujali matokeo/madhara yatokanayo na maamuzi hayo kuenenda kwenye mashauri ya kidunia na kusahau kuwa Mungu ni mkubwa zaidi ya hao tunaowakimbilia. Mtumishi wa Mungu tusisahau kuwa huduma au utumishi ni vita vyenye mapambano lakini utofauti vita hivi vin matokeo ya aina mbili tu tofauti vita vya dunia ambavyo vina matokeo matatu ya ushindi,suluhu na kushindwa ; Vita vyetu ni matokeo ya ushindi na kushindwa na si vinginevyo  kwa hiyo na kwa mtumishi wa Mungu matokeo ni ya aina moja tu pia kwa sababu ya mwanzilishi wetu ambaye naye anatwambia ‘SISI NI WASHINDI SIKU ZOTE’a.UNAPOTESWA ISAYA40; 29Huwapa nguvu waliolegea na huongeza nguvu za wadhaifu.30Hata vijana huchoka na kulegea,nao vijana wanaume kujikwaa na kuanguka,31bali wale wamtumainio BWANA atafanya upya nguvu zao.Watapaa juu kwa mbawa kama tai,watapiga mbio wala hawatachoka,watatembea kwa miguu wala hawatazimia.”b. UNAPOONEWA ISAYA14Kwa haki utathibitika: kuonewa kutakuwa mbali nawe,hutaogopa cho chote.Hofu itakuwa mbali nawe,haitakukaribia wewe.15Kama mtu ye yote akikushambulia, haitakuwakwa ruhusa yangu,ye yote akushambuliaye atajisalimisha kwako.CUMEVUNJIKA MOYO” ISAYA147:3Anawaponya waliovunjika mioyo na kuvifunga vidonda vyao.
  
 2. UMEATHRIKA KATIKA JAMBO FULANI AU TABIA
Watumishi wa Mungu natamani leo tuongelee jambo dogo katika kutamka lakini ugonjwa ambao wa vizazi au urithi ambayo kila mtu ukimpata ana dalili zake tofauti na mwingine ;Maana’ngu ni hii hapa karibu kila mkristo au mtumishi wa MUNGU kuna dhambi inamlazimisha  kuitumikia miaka hadi mingine hawezi kuishinda hadi imefika wakati anakiri hii ni dhambi yangu maana’ke amekata tamaa na ameamua kuitumikia na kusahau kuwa dhambi ni uasi na aifanyanye afanya uasi na pili kuwa atendaye dhambi ni wa shetani na pengine anaweza hata kuitetea akijitafutia haki.Lakini neno la Mungu leo linatukumbusha kuwa haitupasi kuitumikia dhambi bali kuikemea na kuichukia,kwasababu inabeba mauti.Bado kuna nafasi na hakuna haja ya kukata tamaa ya kwenda mbinguni.”RUMI5 ;20Zaidi ya hayo, sheria ilikuja, ili uvunjaji wa sheria uongezeke.”1YOHANA1 ;9Kama tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki, atatusamehe dhambi zetu na kutusafisha toka kwenye udhalimu wote. 10Kama tukisema hatukutenda dhambi, twamfanya Yeye kuwa mwongo na Neno Lake halimo ndani yetu.na YOHANA 8; 36Hivyo Mwana akiwaweka huru mtakuwa huru kweli kweli.

3.NDUGU/JAMAA/RAFIKI WA KARIBU AMEATHRIKA KATIKA ARI AU JAMBO FULANI;
Watumishi wa mungu ebu sasa tukumbushane na hili najua yawezekana ni wewe hata mimi tuna wapendwa  wetu wameathriwa na mambo au hali mbalimbali mfano madawa ya kulevya,sigara,pombe,madeni,uasherati na uzinzi ,lugha chafu na hali nyinginezo hadi tumekata tamaa ya kuwa na ndugu tupendao wenye kunena maneno ya busara. Lakini neno la Mungu leo lasema tusikate tamaa bado kuna njia ya kutokea.Kupitia ushaidi huu.”1YOHANA5;14Huu ndio ujasiri tulio nao ndani Yake, kama tukiomba kitu sawasawa na mapenzi Yake, atusikia. 15Nasi kama tunajua ya kuwa atusikia, lo lote tuombalo, tunajua ya kwamba tumekwisha kupata zile haja tulizomwomba. .

4.UMERUDI NYUMA;
Watumishi wa MUNGU pia wengine yawezekana tumekata tama kisa umeteleza  kiroho hadi unapoona watumishi wenzako unahisi kama wadeni wako ukimwona mchugaji unajificha. Hauna amani hadi umekata tamaa au pengine umerudi nyuma kimaendeleo hadi umefikia kipindi unanena kama wasio amini ,”maendeleo ni ya watu Fulani au Mungu ameniacha au amenisahau au hanipendi .Lakini neno la Mungu linasema usikate tama.Hata kwa wanafunzi yawezekana ufaulu umeshuka Mungu anasema bado kuna njia. “YEREMIA3; 22“Rudini, enyi watu msio waaminifu, nami nitawaponya ukengeufu wenu.“Naam, tutakujia kwa maana wewe ni BWANA, Mungu wetu.” EBRANIA8; 12Kwa kuwa nitasamehe uovu wao,wala sitazikumbuka dhambi zao tena!”1YOHANA1; 9Kama tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki, atatusamehe dhambi zetu na kutusafisha toka kwenye udhalimu wote.

5.MATATIZO KAZINI
  Kila mtu ulimwenguni nadhani anafurahi pale anapofanya kazi  yake  katika mazingira ya utulivu ukizingatia kuwa walio wengi kabla ya kupata kazi upita  mazingira magumu na muda mrefu ,kwa hiyo uhitaji kufanya kazi zao katika hali ya utulivu wa wastani kama sio mazingira mazuri lakini tofauti na yalivyo matarajio ya wengi mambo huwa tofauti ambapo wapo upata matatizo hata pengine zaidi hata enzi kabla ya hizo kazi kwa hiyo watu uamua kuchukua maamuzi magumu kama kwenda kwa wanganga wa kienyeji wakifta msaada na hata watumishi wa Mungu wengine ukata tamaa ya kutegemaea Mungu nao njia za kidunia wakitafta msaada lakini leo Mungu leo Mungu leo anasema nasi kuwa tusikate tama.Kupitia neno lake;”ZABURI55;22Mtwike BWANA fadhaa zako,naye atakutegemeza,hatamwacha kamwe mwenye haki wake aanguke”.1KORINTHO14; 33Kwa Mungu si Mungu wa machafuko bali ni wa amani. Kama ilivyo katika makusanyiko yote ya maana watakatifuWA,WARUMI 8; 28Nasi tunajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hutenda kazi pamoja na wote wampendao, katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi Lake.PAMOJA ZABURI 55 18Huniokoa nikawa salama kutoka katika vita vilivyopangwa dhidi yangu,ingawa watu wengi hunipinga.;

6.LAANA ZA VIZAZI(MABABU)
 Tumekombolewa kwa damu ya mwana kondoo kwa hiyo hakuna haja yoyote ya mtu Mungu kuongopa au kuendelea kuteswa na laana za wazazi au mababu au ukoo vizazi na huku  Yesu Alisha twambia kuwa kwa  kupingwa kwake uponyaji wetu ulipatikana .Ndamu yake ilifuta kila laana na mikosi kwa hiyo mtumishi wa Mungu hakuna sababu ya kuendelea kuteswa na laana kama mfungwa aliyefutiwa makosa lakini bado yuko gerezani toka gerezani kwa kumkumbusha maneno haya;GALATIA 3; 13Kristo alitukomboa kutoka katika laana ya sheria kwa kufanyika laana kwa ajili yetu, kwa maana imeandikwa, “Amelaaniwa yeye aangikwaye juu ya mti.”  

7. MATATIZO YA NDOA
Watumishi wa MUNGU naomba tuongelee jambo ambalo wengi wetu tunakata tamaa kwalo .Pale mwili ulioungnishwa na kristo unapoonekana kuwa na nyufa watu tunaanza kufikilia unakwenda kubomoka baada ya kufikili kuwa bado kuna tumaini la kuziba ! Na wengine tunafikilia kuhama sehemu tukihisi uwezekano wa maisha kuendelea ni mgumu.Lakini leo MUNGU anasema uwezekano wa kuendelea bado upo na pia kufika tuendako ni lazima. Kwa hiyo hakuna sababu ya kuhuzunika au kukata tamaa . Licha ya njia au mapito ambayo mwenzio anakupitisha ,fahamu kuwa ni kitambo tu ;bali una kusudi leo.ISAYA 32: 6Haki itakaa katika jangwa na uadilifu utakaa katika shamba lenye rutuba. 17Matunda ya haki yatakuwa amani, matokeo ya haki yatakuwa utulivu na matumaini milele. 18Watu wangu wataishi katika makao ya mahali pa amani, katika nyumba zilizo salama, katika mahali pa kupumzika pasipo na usumbufu. 19Ingawa mvua ya mawe iangushe msitu 20tazama jinsi utakavyobarikiwa, ukipanda mbegu yako katika kila kijito, na kuwaacha ng’ombe wako na punda wajilishe kwa uhuru. YEREMIA32; 27“Mimi ndimi BWANA, Mungu wa wote wenye mwili, Je, kuna jambo lo lote lililo gumu nisiloliweza?  LUKA 1:37Kwa maana kwa Mungu hakuna lisilowezekana.”

8.WOGA/HOFU ( EBRANIA 13;6Kwa hiyo tunaweza kusema kwa ujasiri, Bwana ni msaada wangu, sitaogopa, mwanadamu atanitenda nini?”)
  Mungu atusaidie watumishi ,natambua wazi kuwa yawezekana kwa hali ya kawaida hakuna mtu ambayo hana hofu katika hali mbaya kwa katka ubinadamu lakini tukitambua kuwa tuna ulinzi wa tofauti wa malaika wa Mungu ambao kila siku wako kazini kwa ajiri yetu.Watumishi wa MUNGU nadhani tofauti na wafalme wa dunia ambao ulindwa na binadamu wenzao ambao mda wowote waweza badilika lakini sisi ufaulme wetu ni wa tofauti kwani MUNGU mwenyewe ndo jemadari katika kuwamuru malaika watulinde sisi kwa hiyo hatuna haja wala sababu ya kuogopa hali au mazingira. 2TIMOTHEO1;” 7Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali roho ya nguvu, ya upendo na ya moyo wa kiasi”.Watumishi pengine tunahofu na wenza wetu tumeshindwa kuaamini ,wakitoka tu mioyo inakuwa juu lakini leo Mungu anasema upendo wa kweli hauna wivu wala hofu.1YOHANA 4; 8Katika upendo hakuna hofu. Lakini upendo ulio kamili huitupa nje hofu, kwa sababu hofu inahusika na adhabu. Kila mwenye hofu hakukamilika katika upendo.

9.MATATIZO YA FAMILIA
 Familia kwa kawaida  ni ile ambayo watoto ,baba na mama na ndugu wengine wanaishi kwa upendo na furaha ikihusisha kusaidiana lakini ,tofauti na matarajio familia nyingi hiyo hali imekuwa ya kusoma katika vitabu vya historian a kwao wazazi wapo lakini ni yatima na wazazi wanakuwa wajane na wagane wenza wao wakiwa bado hai .Ndugu kwa ndugu wanaishi visiwani wakiwa hakuna usafiri wa majini au daraja  ili wakutane.Lakini leo mungu anasema bado kuna nafasi na njia kwa sababu,amejenga daraja na kuvunja kuta kati yenu.ISAYA 32; 17Matunda ya haki yatakuwa amani, matokeo ya haki yatakuwa utulivu na matumaini milele.18Watu wangu wataishi katika makao ya mahali pa amani, katika nyumba zilizo salama,katika mahali pa kupumzika pasipo na usumbufu.KUMB 26; 11Kisha wewe pamoja na Walawi na wageni wote walioko miongoni mwenu mtafurahi katika vitu vyote vizuri ambavyo BWANA Mungu wenu amewapa pamoja na wa nyumbani mwenu.ZAB127;1BWANA asipoijenga nyumba, wajengao hufanya kazi bure.BWANA asipoulinda mji,walinzi wakesha bure

10.UNAPOFIWA NA MPENDWA WAKO
 Kiubinadamu huwa ni vigumu sana kutoonesha huzuni ,kuweweseka ,kukosa kula,kukosa kuamini uakika wa kuwa salama kesho pale tunapopoteza wapendwa wetu na mara nyingi ikitokea ni zaidi ya mara moja au kupoteza wapendwa wengi kwa wakati mmoja pengine tunaweza kupingana na Mungu katka maneno yake ktk ISA 49:15 na kusahau kushukuru hata kwa yale aliyotusaidia katika mapito hayo. Lakini leo Mungu anasema bado lango la matumaini liko wazi.MATAYO5; 4Wana heri wale wanaohuzunika,maana hao watafarijiwa.2KOR1; 3Ahimidiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa huruma na Mungu wa faraja yote. 4Yeye atufarijiye katika taabu zetu zote, ili tuweze kuwafariji wale walio katika taabu yo yote kwa faraja ambayo sisi wenyewe tumepokea kutoka kwa Mungu.ZABURI147; 3Anawaponya waliovunjika mioyo na kuvifunga vidonda vyao.

11.GUVU ZA GIZA
Mpendwa nadhani sio mara ya kwanza kusikia neno nguza giza au nguvu za mapepo ambapo baadhi ya watu wanaendelea kuteseka kwa sababu ya nguvu hizo ,familia hakaliki kwa sababu ya nguvu hizo. Pia wanafunzi wameachishwa shule kwa sababu hiyo ,hadi tumefikia kipindi tumeamua kwenda kwa wachawi/waganga wa kienyeji kutafuta na kusahau Mungu ambaye ndiye aliumba hata hao waganga. Lakini leo MUNGU leo anasema kuwa bado kuna lango na hakuna haja kukata tamaa.LUKA10; 19Tazama nimewapa mamlaka ya kukanyaga nyoka na ng’e na juu ya nguvu zote za adui, wala hakuna kitu cho chote kitakachowadhuru kwa namna yo yote. YAKOBO4;7Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.YOHANA8; 36Hivyo Mwana akiwaweka huru mtakuwa huru kweli kweli.
  
HITIMISHO
 Watumishi wa Mungu mbarikiwe sana na malaika wa Mungu wako zamu kuwalinda wala msiwe na hofu kwa sababu wanatimiza wajibu wao ambao Mungu amwamuru kufanya .Pia mtumishi tumtumikie Mungu kwa uaminifu naye hatatuacha bali ataendelea kututumia kwa kusudi lake kwasababu ni ahadi yake kwamba atatimiza ahadi kuliko hat neno lake tusimsahau wala kusahau kazi yake YEREMIA2; 32Je, mwanamwali husahau vitu vyake vilivyofanyizwa kwa vito,bibi arusi husahau mapambo yake ya arusi? Lakini watu wangu wamenisahau mimi,tena kwa siku zisizo na hesabu.
usikate tamaa